TAA: Hakuna ajali yoyote ya Ndege eneo la Ziwa Victoria

TAA: Hakuna ajali yoyote ya Ndege eneo la Ziwa Victoria

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Mussa Mbura amesema hakuna ajali ya ndege leo kwenye Ziwa Victoria Jijini Mwanza bali kilichofanyika ni mazoezi ya utayari.

Mussa Mbura amesema yafuatayo "Haya ni mazoezi ya kujiweka tayari ambayo tumeendelea kuyafanya, kama Mamlaka za Viwanja vya Ndege miongozo inatutaka tuwe tunafanya mazoezi ya mara kwa mara kuhakikisha Watu wetu wapo tayari pale inapotokea tatizo kila Mtu kwenye eneo lake awe tayari"

"Serikali ina Airport inazoziendesha takribani 58, haya mazoezi yanatakiwa yafanyike kwenye Airport zote hizo ndio maana mnaona series ya mazoezi kwenye Airport tofauti ndio maana tumefanya Kahama na leo tumefanya hapa Mwanza, kwahiyo hakuna ajali halisi leo kama inavyoripotiwa ni mazoezi tu ya utayari"

1677153201196.png
 
Ikitokea yenyewe kama yenyewe sasa,ni mpaka kina Majaliwa watokee,haya mazoezi ya uokoaji wawe wanawapa wavuvi maana wamekuwa ndiyo wafikao haraka zaidi kuliko kikosi cha zima moto.
 
Wawe wanatangaza kabla ya zoezi.

Kama ni utayari basi wasiifanye iwe taharuki (kiki), maana utayari ni sehem ya kazi na wajibu wao.
 
Ignorance ignorance ignorance!!!!

Ajali huwa inatokea kwa kushtukiza wala haisubirii uwe tayari kui zuia isitokee...

Kuandaa Ajali ya kujifunza halafu ujiweke tayari, ujiandae kwa ajili ya uokozi ina maanisha hamna kinacho fanyika maana tayari unajua nini cha kufanya na eneo husika la "Ajali ya mafunzo" itakapo kuwa located..

Vipi je iki anguka msituni huko, Au mtoni, Au katikati ya bahari sehemu ambayo hatu dhanii kwamba hapa inaweza kutokea ajali ya ndege?

Uokozi utafanyika kwa muda??

Kwa mtazamo wangu wanacho kifanya hawa eti " mazoezi ya utayari" ni ujinga.

Ajali haina specific location ya kutokea.

Ndege ya Nepal ile ilianguka korongoni.

Na sijua kama nchi zingine hufanya hivi kuangusha ndege za majaribio ya uokoaji..
 
Back
Top Bottom