RESOLVED KERO Taa nyingi za kuongoza magari Barabarani KATAVI hazifanyi kazi zaidi ya miezi mitatu sasa

RESOLVED KERO Taa nyingi za kuongoza magari Barabarani KATAVI hazifanyi kazi zaidi ya miezi mitatu sasa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hali ya taa za barabarani ambazo zimeungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu.

Tatizo hili limekuwa kubwa hasa kwa watembea kwa miguu wanaotumia barabara nyakati za usiku. Baadhi ya maeneo yamebaki bila mwanga kwa muda mrefu, hali inayosababisha hofu na changamoto za kiusalama kwa wananchi.

Mfano ni eneo la barabara ya Makaburi ya Waarabu hadi Madukani, za Stendi Kuu ambako taa za barabarani zimeharibika na hazifanyi kazi. Pia taa kubwa ya kuongoza magari katika eneo hilo imeungua na imekuwa katika hali hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu bila kufanyiwa matengenezo.

Hali hii siyo tu inawaathiri watembea kwa miguu, bali pia madereva wanaotumia barabara hizo hasa nyakati za usiku, kwani ukosefu wa mwanga unaweza kuongeza hatari ya ajali na matukio mengine ya kiusalama.

Tunaiomba mamlaka husika zikiwemo serikali ya mkoa na wahusika wa miundombinu ya barabara kufuatilia changamoto hii na kuhakikisha taa hizo zinatengenezwa ili kurejesha usalama na urahisi wa matumizi ya barabara kwa wananchi.

Soma Pia: Baadhi ya taa za barabara kwenye barabara ya Sanawari - Ilboru, Tanki la Maji - Mollel hazifanyi kazi, zimekuwa kero

Taa za barabarani ni sehemu muhimu ya ulinzi na usalama wa wananchi, hivyo tunashauri matengenezo yafanyike kwa wakati ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza.
photo_2026-08-04_11-52-36.jpg
photo_2026-08-04_11-52-35 (3).jpg
photo_2026-08-04_11-52-35 (2).jpg

Pia soma ~ TANROADS yafunga taa mpya za kuongoza magari Mkoani Katavi baada ya zile za awali kuharibika
 
Back
Top Bottom