Taa ya ABS kuna muda inawaka, muda mwingine inazima!

Wakuu msaada kipi nifanye, gari ni Mazda Axela, brake zinafanya kazi fresh! Ila imewahi funguliwa kwa ajiri ya kuweka spacer!
Taa ya ABS inapowaka na kuzima inaweza kuashiria matatizo kama kiwango cha chini Mafuta ya Breki au Pipe hazipeleki Mafuta ya Breki vizuri, Sensa ya Speed ina tatizo (Imeharibika), kuna hitilafu ya umeme, kuna Fuse inachomoka na kujigusa tena au waya zisizokuwa na muunganiko mzuri.

Kama taa itaendelea kuwaka baada ya kuwasha injini, inamaanisha kuna tatizo kwenye mfumo wa ABS ambalo linahitaji kushughulikiwa haraka kwa sababu ABS ni kipengele muhimu mno kwenye usalama wa gari yako.
 
Asante mkuu nitafanyia kazi
 
Hii huwa ina maana zaidi ya moja kama walivotangulia wadau hapo ikihusisha brake na matairi. Iliwahi kunikuta nikarudisha gari nikaenda job siku nzima nagoogle tu hahaha. Nikakutana na wataalamu wa YouTube jamaa wanasema kitu cha kwanza nicheki upepo ebwana eeh kumbe lile ndo lilikuwa tatizo nlikuwa natembea na upepo mdogo kinoma.

Since that day sijaona tena ikiwaka miezi sasa na nimekuwa nikicheki upepo mara kwa mara japo nafikiria nikaweke Nitrogen ili nisipate heka heka nyingi.
 
Mkuu sijaleta tu mrejesho ila na mimi issue ilikuwa upepo, maana na Taa ya Traction control kuna muda ilikuwa inawaka, nilivyogoogle hiyo nikakuta inasababishwa na upepo mdogo na ndo inapelekea pia mpaka ABS kuwaka! Nilivyojaza upepo zote zikazima na hazijawaka tena.

Hap fundi alikuwa anaelekea kunipiga hela maana alisema tucheki kwenye mashine kwa 50k , nikamwambia angoje kwanza. Vipi kuhusu nitrogen inakuwaje hiyo!?
 
Hapo safi mkuu Google inasaidia sana mi nlimpa jamaa buku 2 akaweka upepo biashara ikaisha.

Nitrogen ni upepo ambao hauathiriki na joto au baridi kama unavojua matairi yanatabia ya kutanuka na kusinyaa kipindi flani kama unatumia upepo wa kawaida so Nitrogen yenyewe haina hiyo tabia.
 
Kwamba hiyo nitrogen unaweka kwenye matairi?

Kwani huku upepo tunaojaza kwenye vituo vya kujaza upepo ni gesi gani?

Hiyo Nitrogen vituo maalum vya kujaza ? Na gharama zake?

Kuna matairi spesho ama tairi zozoge unaweza kujaza?
 
Back
Top Bottom