⚠️Taa ya check engine inawaka na gari inakosa nguvu , msaada !

⚠️Taa ya check engine inawaka na gari inakosa nguvu , msaada !

Boss wahi garage baraka hiyo taa ni hatari kwa gari yako. Kama bado unaliendesha lisogeze home uite mafundi walicheki kama kuna garage ya karibu jaribu kuuliza wafanya preliminary diagnosis.


Sijui gari yako ina shida gani ila hiyo taa ya check engine sio ya kupuuza.
 
Habari ! Jioni hii baada ya kupiga presha (ndan ya Bonet kupunguza Vumbi) ,gari yangu imeanza matatizo haya :-
---Taa ya Chek Engine inawaka bila kuzima
---Taa ya O/D (overDrive) inajiwasha na kujizima bila hata kugusa button yake ya kuwasha
---Gari imekosa nguvu kabisa na inachelewa kubadili Gia
Naomba msaada wenu wadau nini yaweza kuwa shida kwenye gari au ni kifaa kipi kitakuwa kimekufa .

Maswala ta kupiga pressure engine espnya petrol,, usijaribuuu,, hata muoshaji aseme anaiacha inawaka.. kuna vitu sensi mtive mule,,

Engine ya petrol yapigwa pressure na petrol
Engine ya diesel yapigwa pressure na diesel

Sio MAJI..

Kacheki sparkplugs utakuta zimeingia maji inapona
 
Usipige presha yenye maji kwenye Engine piga ya upepo mkavu tena usiwe mkali
 
mkuu achana na ramli.... nenda garaje kafanye computer diagnosis tatizo lijukikane

matatizo ya kimfumo usipende kuyatibu kwa ramli wala kupeleka kwa mafundi wa chini ya muembe...

peleka garaje inayoeleweka fanya diagnosis...

hawa mafundi wa chin miembe huwa ukiwapelekea wanachofanya wanakata fuse ili hyo taa isiendelee kuwaka na tatizo linabaki palepale sema tu taa inakuwa haiwaki maana wamekata waya
 
Habari ! Jioni hii baada ya kupiga presha (ndan ya Bonet kupunguza Vumbi) ,gari yangu imeanza matatizo haya :-
---Taa ya Chek Engine inawaka bila kuzima
---Taa ya O/D (overDrive) inajiwasha na kujizima bila hata kugusa button yake ya kuwasha
---Gari imekosa nguvu kabisa na inachelewa kubadili Gia
Naomba msaada wenu wadau nini yaweza kuwa shida kwenye gari au ni kifaa kipi kitakuwa kimekufa .

••••••UPDATES •••••
Asanteni ,nime-solve tatizo kuna waya mmoja ulilegea tu ,now iko fine .
 
Salaam wadau. Check engine ya Toyota Coaster; Model HDB50, Engine 1HFE inawaka na kupoteza nguvu (accelerator haivuti). Kuwaka ni hino moja, inaweza tembea km kadhaa bila tatizo, ghafla taa inawaka na gari kupoteza nguvu. Nimeipeleka kwa wataalam wenye On-Board Diagnostic kit na kutoa codes kama inavyoonekana. Mtaalam amejaribu kufatilia hiyo kitu bila majibu chanya. Naomba msaada kwa mwenye utaalam wa kuzitambua hizo codes
 

Attachments

  • IMG_20190430_170839.jpg
    IMG_20190430_170839.jpg
    101.9 KB · Views: 68
  • IMG_20190430_170836.jpg
    IMG_20190430_170836.jpg
    151.8 KB · Views: 65
  • IMG_20190430_170833.jpg
    IMG_20190430_170833.jpg
    152.7 KB · Views: 67
Kwanini usituandikie hizo Codes maana hazisomeki vizuri.
 
Trouble codes ni
1. Code iliyosoma gari ikiwa imesimama, gari linawaka na taa ya check injini ikiwaka ni

P1123: Current: Accel. Closed Position SW Circuit (Open)

2. Code iliyosoma tukiwa tunatest gari na ghafla taa ikawaka ni

P1122: Current: Accel. Position Sensor Circuit (IDL SW/Range)
 
Back
Top Bottom