Responded TAA yatangaza viwango vipya vya gharama za maegesho ya magari Uwanja wa Ndege Dar (JNIA)

Responded TAA yatangaza viwango vipya vya gharama za maegesho ya magari Uwanja wa Ndege Dar (JNIA)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
#taarifa (1).jpg

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA
29 Septemba, 2026

YAH: GHARAMA YA MAEGESHO YA MAGARI KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA JULIUS NYERERE (JNIA)


Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inapenda kuutaarifu Umma kuhusu gharama mpya za maegesho ya magari katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) mara baada ya usimikaji wa mfumo mpya wa maegesho ya magari.


Gharama hizo ni kama ifuatavyo:
GHARAMA ZA MAEGESHO – JNIA (kuanzia 29 Septemba 2026)

1. Malipo kwa saa ya kwanza
- Gari la abiria: TZS 3,000/=
- Mini Bus au Van: TZS 5,000/=
- Basi au Lori: TZS 10,000/=
2. Kila saa ya ziada (magari yote): TZS 1,000/=
3. Maegesho ya muda mrefu (Long-Term Parking)
- Siku 1–7: TZS 25,000/=
- Kuanzia siku ya 8: TZS 15,000/=
4. Maegesho yasiyo sahihi: TZS 50,000/=
5. Kupoteza kadi ya maegesho: TZS 30,000/=
6. Kukwepa malipo ya maegesho: TZS 50,000/=
7. Teksi zisizoidhinishwa: TZS 100,000/=
8. Kuendesha kwa mwendo kasi: TZS 30,000/=

TAA inapenda kuwakumbusha Watumiaji wa viwanja vya ndege kuzingatia taratibu, kanuni na maelekezo yanayotolewa ili kuhakikisha usalama, na huduma bora kwa abiria na Wadau wa viwanja vya ndege.


Imetolewa na:


KITENGO CHA UHUSIANO KWA UMMA NA MAWASILIANO
MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA



Pia soma ~ Taksi Mtandao hatutendewi haki maeneo ya Uwanja wa Ndege Dar, tunapigwa faini za ajabu na kuitiwa Polisi
 
Back
Top Bottom