KERO Taa za Barabarani (Solar) zilizofungwa na TANROADS Sumbawanga Mjini zina mwanga hafifu unaoweka Kivuli badala ya kuangaza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
TanRoads Rukwa hebu kueni na consistency kwenye specifications zenu.

Inakuaje Taa Mpya mlizofunga Sumbawanga Mjini na Kijiji Cha Chala na Kaengesa huko hazitoki Mwanga wa kutosha muda wa usiku?

Ieleweke hizo taa sio mapambo bali ni kusaidia usalama na Biashara muda wa usiku, Sasa zinaposhindwa kutimiza wajibu huo inakuwa haina maana na pesa za walipa kodi zimelipwa.

Iweje taa mlizofunga mwaka juzi zinawaka vizuri ila mlizofunga mwaka huu haziwaki vizuri na zina mwanga hafifu ambao unaweka kivuli usiku badala ya kuangaza?

My Take
Kajifunzeni TanRoads Katavi wao taa zao zinawaka Mji mzima na Vijijini kote walikozifunga, nyie wa Rukwa Vitaa vichache halafu haviwaki.

Mamlaka husika wakalitazame hili.
 
kumbe huwajui watu wa huko, washafanya yao
 
Wananunua zile zilizotupwa china
Tutalalamika mpaka kiama kifike
Hatuwezi kutengeneza vya kwetu hata ndege wanatushinda kutengeneza viota vyao hopeless kabisa
 
Wananunua zile zilizotupwa china
Tutalalamika mpaka kiama kifike
Hatuwezi kutengeneza vya kwetu hata ndege wanatushinda kutengeneza viota vyao hopeless kabisa
Hakuna wadhibiti viwango ndani ya taasisi? Viongozi wengine wa Kiserikali wenye dhamana hawaoni huu uhuni?
 
Bora zenye mwanga hafifu utajua kuna taa Morogoro nyingi zimekufa na no replacement
 
Basi tutakuwa ni jamii ya ajabu sana
Hakuna wa kuweza kudhibiti maana imekuwa ndio system ya hivyo
Mkuu tuache ushabiki pembeni je umewahi kuona kitu gani kinafanyika bila kasoro zozote au upigaji
Mara mnalalamika Vyoo vya stendi vichafu kwani walipokuwa wanajenga hawakujua vinahitaji waangalizi 24/7?
Au mishahara inaliwa na wajanja tu
Shule zilivyo mpaka huruma na sisi wananchi hatuna neno tunaenda tu
Ukienda mahospitali ndio kabisa
Kote huko kunahitaji hela na ndio hizo zinapigwa
Angalia majuzi askari walivyomwagwa kila kona ya nchi kulinda usalama na kuzuia maandamano
Unajua ni kiasi gani cha fedha kilitumika kwa siku 2 hizo ?
Sasa wenzetu majuu ndio kazi zao za kila siku kuwepo kila sehemu ya nchi wakitulinda na yote hiyo ni pesa zinazofanya kazi kwa halali
 
Bora zenye mwanga hafifu utajua kuna taa Morogoro nyingi zimekufa na no replacement
Sijajua kama Mamlaka Huwa wanaweka za nini kama hawawezi kizifanyia maintanance
 
Labda jua linawaka mwisho Mbeya mjini.Fuatilia.
NB:Ni za solar power siyo?
 
wee unafikiri sumbawanga mchezo nini?,,,,,,,,,unataka izo taa zimulike mawizadi?????,,,kule pikipiki fisi,ndege ungo,fuso kasongo!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…