A
Anonymous
Guest
Serikali imeweka mfumo wa taa za kuongozea magari (traffic lights) katika eneo la Mombasa, Ukonga, kwa lengo la kupunguza ajali na kuimarisha usalama barabarani. Hata hivyo, bado kuna changamoto kubwa ya kutokuzingatiwa kwa taa hizo na baadhi ya madereva pamoja na watumiaji wengine wa barabara.
Kutokana na ukosefu wa usimamizi wa kutosha, ukiukwaji wa sheria za barabarani umeendelea, hali inayochangia kutokea kwa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo.
Tunaomba Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na mamlaka husika kuongeza usimamizi na kuchukua hatua dhidi ya wanaokiuka matumizi ya taa za kuongozea magari ili kufanikisha lengo la kuimarisha usalama wa watumiaji wa barabara.