Taa za umeme za LED huleta nafuu katika bili ila ni hatari kwa afya

Mimi nileshakuwa addict wa LED. Mwanga Murua kabisa. Hasa nyumba ikiwa umepaka rangi nyeupe.....Safiiii. Yaani inapendeza sana.
Mkuu kumbe tupo wengi mimi pia ni muhanga wa uraibu wa hizi taa yani sipati usingizi kabisa nisipoacha taa ikiwa on yani naweza kulala vizuri kwenye mazingira yenye mwanga (LED in particular) kuliko nikiwa gizani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Siasa inaua
2. Kujamiana kunaua
3. Dini inaua
4. Biashara inaua
5. Pesa inaua
6. Starehe zinaua
7. Pombe inaua
8. Kazi inaua
9. Chakula kinaua
10. Taa za LED zinaua
11. Vinywaji baridi kama coca, red bull nk vinaua
12. Sukari inaua
13. Dawa zinaua ( the best medicines are dangerous poisons)
nk
Kila kitu hapa Duniani kina hasara na faida.
Kwa hiyo tunapofanya jambo fanya kwa kiasi na kama ukifanya unapata madhara , acha kabisa.
Kama ukiacha unakufa haraka zaidi basi endea kufanya hadi utakapokufa.
PIa Serikal (TBS) iko kwa ajili ya kumlinda mlaji kwa vitu vinavyotengenezwa viwandani. Kwa hiyo kama hawajatoa tahadhari hatuna haja ya kuwa na wasi wasi
 
Kuna zile naona zimetengenezwa kama tubelight zina plastic kuzuia zile led zenyewe usizione moka kwa moja, je hii haisaidii kupunguza hizo athari?
 
acha kudanganya watu wewee, taa za tubelight zina madhara makubwa sana ukilinganisha na LED, teknolojia yake inatumia mercury, sijui kama unajua kwenye bulb za tubelight ( zile mtaani tunaziita energy saver) hutakiwi kabisa kuigusa hiyo bulb, na unapo nunua kuna onyo/katazo la kutoshika hizo taa 'with bare hands'
 
Kwa sasa vifaa vya electronics ambavyo ni high quality wamekuwa wakifilter blue light.

Hasa hili nimeliona kwenye simu TV na computers...

Sent using Jamii Forums mobile app


Ni kweli kabisa maana nilipata shida ya macho nikajua moja kwa moja tatizo linasababishwa na matumizi yangu ya laptop, nilivyoenda hospitali (ccbrt) daktari alinipima akaniambia sababu tofauti kabisa na niliyokua nafikiria.

Ikabidi nimwambie kuhusu matumizi yangu yaliyokithiri ya laptop, akaniambia mwanga wa vifaa vingi vya kielectronic vya kisasa hauna madhara kama watu wengi tunavyodhani. Akanipa mfano wa computers ambazo zilikua na athari kidogo kwenye macho ni zile za kizamani ambazo mwanga wake ulikua unachezacheza.

Nakumbuka huyu daktari alikua myahudi sio mbongo!
 
Hizo ni salama ukilinganisha na LED
Kwani Transistor hizo energy saver si ndio hizo Led, ambazo zimeitwa Energy saver kwa kuwa power consuption yake ni ndogo sana ulilinganisha na zile taa za mwanzi au zile bulb za kizamani?
Halafu hizi Led ziko zile zina muwako wa warm light je nazo zina madhara kama hizi zenye muwako mweupe?
 
Na manga wa kibatali nasikia unaongeza nguvu za kiume
 
Mimi nina umri wa miaka 82 mpaka macho yaharibike nitakuwa sina hamu ya kuona mabinti wazuri hivyo sina cha kupoteza. Kichwa kuuma si rahisi sina kazi hivyo ninashinda nakunywa mbege, sijui kitaanzia wapi! Usingizi utapatikana tu nikisha kata mbege kutwa nzima. My mbege, my dear bottle.
 
Afadhali kuna good news
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…