Kabisa. Watu wananunua hizi bulb za bei nafuu halafu wanalalamika. Hivi huwa wanaona bulb za VX, Prado, toyota land cruiser, Discovery, Harrier new model, Mercedes benz, BMW, VW ikipigwa low beem unaona hadi ramani ya Africa.
Sasa jiulize akipiga full itakuwaje. Na zile taa huwa zinakuja na lenzi yake. So ikiwashwa inalenga on point inapomulika so hakuna umande utaiblock hiyo beam.
Vijana wazito sana kujifunza. Changamoto kidogo tayari wanatoa conclusions badala ya kutuliza kichwa kudadisi shida imeanzia wapi.
Ndo maana wengi magari ya kiume yanawashinda wanapenda brand nyepesi kutumia kama Toyota maana hawataki kunoa akili zao na kuyajua magari.
Kuna ndugu yangu ni dereva alikaa na mzungu kwenye gari yake namna alikuwa naifuatilia alikuwa anaijua kuliko yule mzungu sasa ukikuta anamuelekeza utacheka maana uona mbongo anamfunza mzungu kuhusu gari na hatuna hata kiwanda cha magari [emoji23][emoji23][emoji23]