Kumekuwa na majigambo mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa wapenzi na mashabiki wa klabu tajwa hapo juu, kwamba kesho wanaua. Napenda kuwashauri, hayo matokeo waliyokuwa nayo waanze kuyafuta vichwani mwao tangia sasa, maana matokeo ya mchezo wa kesho yanaweza kuwa kinyume na matarajio yao hivyo ikwaathiri kisaikologia na ikapelekea kufanya mambo kinyume na utaratibu kama ilivyowahi tokea siku za nyuma. Nadhani wale wapenzi wa mpira mmenielewa. Asanteni kwa kuzingatia hili angalizo.