Wakubwa mi ninasikitishwa sana na hali ya taaluma inapoelekea tanzania. kwani elimu ya sasa sio, yaani watu wanapewa vyeti tu na sio taaluma na ndio maana wengi tunamaliza vyuo vikuu tunasambaa mitaani bila ajira, hi ni kwa sababu hatuna taaluma tuna vyeti hivyo ata kujiajiri inakua ndoto.utajiajiri vipi wakati huna taaluma? yani mtu anamaliza chuo hata kingereza cha kuomba maji inakua shida wakati wenzetu waliomaliza miaka ya 1992 kushuka chini walikua bora na walikua wanatofautiana kabisa na mtu ambaye hajahimu. hii inatokana na nini? kufundishwa na waliofeli, usimamizi mbovu, walimu kufuata maslai zaidi, uzembe wa wanafunzi, mitaala mibovu, uongozi mbovu, wanafunzi kuanza shule na umri mdogo, ufisadi, vipimo vibovu vya uelewa au nini?