Taaluma Tanzania

Taaluma Tanzania

kitumanga

Member
Joined
Aug 16, 2011
Posts
45
Reaction score
4
Wakubwa mi ninasikitishwa sana na hali ya taaluma inapoelekea tanzania. kwani elimu ya sasa sio, yaani watu wanapewa vyeti tu na sio taaluma na ndio maana wengi tunamaliza vyuo vikuu tunasambaa mitaani bila ajira, hi ni kwa sababu hatuna taaluma tuna vyeti hivyo ata kujiajiri inakua ndoto.utajiajiri vipi wakati huna taaluma? yani mtu anamaliza chuo hata kingereza cha kuomba maji inakua shida wakati wenzetu waliomaliza miaka ya 1992 kushuka chini walikua bora na walikua wanatofautiana kabisa na mtu ambaye hajahimu. hii inatokana na nini? kufundishwa na waliofeli, usimamizi mbovu, walimu kufuata maslai zaidi, uzembe wa wanafunzi, mitaala mibovu, uongozi mbovu, wanafunzi kuanza shule na umri mdogo, ufisadi, vipimo vibovu vya uelewa au nini?
 
Yani wewe uandishi wako ni mbovu na sidhani kama unaufahamu kuwa ili ni jukwaa ni la wasomi na unapaswa kutumia lugha ya kistaharabu na inayoelewa,nini maana ya kinyama? Au m2? Rudia upya huu uzi maana msomi hawezi kujadiliana mambo kwa lugha za kiuni.NATUMAINI UMEELEWA.
 
haya nimerekebisha mkubwa. vipi we mwalimu nini?
 
kuna mtu humu-nadhani mwanakijiji- alishasema watanzania tujifunze kuishi kulingana na maamuzi ya uchaguzi tuliyoyafanya. so mkuu usishangae sana. Kama hata rais wako hajui nini chanzo cha umasikini wa watu anaowaongoza unategemea nini?
 
haya nimerekebisha mkubwa. vipi we mwalimu nini?

swala la kuwa mwalimu au raha linauhusiano gani na kukutaka utumie lugha ya kistaharabu?? Au unataka kujua taaluma yangu tu?? Achana na mawazo mgando kuwa kundi fulani la watu mfano wachungali,walimu na mashekhe ndio wanathamini lugha iliyo safi maana kuna baadhi ya mateja(wala unga) wanajali pia matumizi ya lugha bora.
 
Kwa uelewa wangu mdogo nadhani tatizo kubwa ni kwa wanafunzi wenyewe tokana na sababu zifuatazo.

1. Wanafunzi wengi wa elimu ya juu wana mawazo mserereko na hawapo tayari kujifunza mambo mengine ya zaidi ya yale wanayofundishwa drsn.
2. Baadhi ya mavazi yanayovaliwa yameshusha thamani ya elimu ya juu kwani hayana mfano wa kuigwa na kujenga picha ya kisomi.
3. Wanafunzi wanawaza kukariri na kufaulu mitihani badala ya kuwaza kuelewa mabo wanayofundishwa.
4. Baadhi ya wanafunzi husoma kozi kama fasheni ili nae aonekane kuwa yupo chuo kikuu kwenye jamii inayomzunguka.
5. Kukosa miongozo wakati wa kuchagua shahada za kujifunza na kutoangalia background ya familia atokayo.
6. Kundekeza starehe ambazo alikuwa hana uzoefu nazo kutokana na mazingira aliyotokea
. n.k n.k n.k
 
Mkuu ni kweli uliyoyasema,bt ukumbuke kuwa mazingira ndio yanayomuonga na hata kumbadilisha mtu,sasa kutkna na mfumo wa elimu uliopo nchini kwetu c ajabu kuyaona hayo yote uliyoyaorodhesha yanatokea ktk vyuo vyetu.
 
Yani wewe uandishi wako ni mbovu na sidhani kama unaufahamu kuwa ili ni jukwaa ni la wasomi na unapaswa kutumia lugha ya kistaharabu na inayoelewa,nini maana ya kinyama? Au m2? Rudia upya huu uzi maana msomi hawezi kujadiliana mambo kwa lugha za kiuni.NATUMAINI UMEELEWA.

swala la kuwa mwalimu au raha linauhusiano gani na kukutaka utumie lugha ya kistaharabu?? Au unataka kujua taaluma yangu tu?? Achana na mawazo mgando kuwa kundi fulani la watu mfano wachungali,walimu na mashekhe ndio wanathamini lugha iliyo safi maana kuna baadhi ya mateja(wala unga) wanajali pia matumizi ya lugha bora.

Hili
Kistaarabu
Wachungaji.
 
Kwa uelewa wangu mdogo nadhani tatizo kubwa ni kwa wanafunzi wenyewe tokana na sababu zifuatazo.

1. Wanafunzi wengi wa elimu ya juu wana mawazo mserereko na hawapo tayari kujifunza mambo mengine ya zaidi ya yale wanayofundishwa drsn.
2. Baadhi ya mavazi yanayovaliwa yameshusha thamani ya elimu ya juu kwani hayana mfano wa kuigwa na kujenga picha ya kisomi.
3. Wanafunzi wanawaza kukariri na kufaulu mitihani badala ya kuwaza kuelewa mabo wanayofundishwa.
4. Baadhi ya wanafunzi husoma kozi kama fasheni ili nae aonekane kuwa yupo chuo kikuu kwenye jamii inayomzunguka.
5. Kukosa miongozo wakati wa kuchagua shahada za kujifunza na kutoangalia background ya familia atokayo.
6. Kundekeza starehe ambazo alikuwa hana uzoefu nazo kutokana na mazingira aliyotokea
. n.k n.k n.k

Hayo yote ni sababu sahihi sina la kuongeza
 
Back
Top Bottom