Taaluma ya UDOM manufaa yake ni madogo sana kwa jamii

Kalinzi

Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
86
Reaction score
14
TAALUMA YA UDOM HAINA UKOMBOZI

Wadau wa JF,

Napenda naomba kutoa mawazo haya wazo ingawa najua wazi kuwa yatawauma walio wengi hususani kwa wale wenye watoto katika chuo hicho au wengine wanaosomea hapo moja kwa moja.

Tokea chuo hicho kianzishwe mnamo wa mwaka 2007 na mazao yake kuanza kupatikana mwaka 2010 hakuna mwanafunzi mmoja aliyeweza kusimama na kujinadi katika chaguzi mbalimbali hususani za 2010 na hata katika chaguzi ndogondogo zinazotarajiwa kufanyika feb 2 2014 hakuna hata jina moja ambalo liko tarajali kuingia katika kinyanganyiro hicho.

Kwa kuwa matumaini makubwa ya watanzania ni kuona wasomi wanakuwa chachu ya mabadiliko na ujenzi wa jamii mpya kiuchumi, kitamaduni hata kisiasa je wanafunzi hawa wanaomaliza katika chuo hicho hawana uwezo kiasi cha kutoweza kusimama mbele za watu?
Elimu inayotolewa hapo haina viwango vya kumuandaa mwanachuo kiasi cha kushindana na soko la sasa la ajira ambalo kwa sasa linakimbilia kwenye siasa?

inakuwaje vyuo vyenye wanafunzi wachache vinakuwa na ushawishi sana mtaani kisiasa na kijamii ukilinganisha na chuo hiki kinachochukua maelfu ya wanafunzi kwa mwaka hivi uongozi wa hapo haujashtuka kuwa huenda elimu inayotolewa hapo haiendani na matakwa ya maisha ya KITANZANIA ya sasa?

NAWASILISHA

Source: utafiti binafsi na wanafunzi wanaosoma UDOM
 
Siasa ni ajira? Wewe pia unaonekana umepitia hapo UDOM na ukakatwa bugi! Pole.
KY, hata hao inaowajua wahitimu UDSM ni balaa tu mitaani na kwenye Sihasa.
 
we msomi wa wapi unaetoa uchambuzi dhaifu hivi?
Tangu lini siasa ikawa ajira?

Pole kwa kukosa nafasi udom, kukiponda hakutosaidi.
Wenzako wanamaliza wanasogea hatua nyingine ktk maisha.
We baki kulalama na kukosoa.
 
utafiti dhaifu,Mawazo dhaifu! Jipange ndio ulete tena huo uzi,Kwani kila anayesoma UDOM ni lazima awe mwanasiasa? Umekariri!
 
Kwani hicho Chuo kinaitwa University of Dodoma (UDOM) au Islamic University of Dodoma?Just asking!
 
Udom ni makada wa ssssssm tu, ina vilaza wengi just gentle pass!
 

Pole sana maana najua hapo ndo mwisho wako wa kufikiri
 
Udom ni makada wa ssssssm tu, ina vilaza wengi just gentle pass!

Kumbe ndio maaana kwenye mtihani wa form six wanaandika namba ya uanachama na chama cha mtahiniwa!!!!

We jamaa una kipaji asee why not join futuhi or ze comedy????!!!
 
Kwa akili zako kuitumikia jamii ni kwenye siasa tu? Kuna hao wasomi wako wamejaa jukwaa la siasa humu jf wanatoa hoja gani zaidi ya kutoa pumba? We jamaa jinga sana.
 
Mbulula wewe nenda kamuulize Waziri wenu wa elimu kijana aliyetaka kumuharibia ubunge wake 2010 ni nani atakwambia, tena kijana Habibu Mchange akiwa mwaka wa pili alichakachuliwa ubunge wake kamuulize Kawambwa anamjua vizuri, chuo kikiwa na umri miaka mitatu kijana alijitokeza kugombea kupitia CDM tena akiwa bado hajamaliza masomo yake, kwa great thinker huu ni ujasiri wa hali ya juu, kijana mwingine Alex Mushi akiwa mwaka wa tatu aligombea ujumbe wa BAVICHA akashinda kwa kishindo, Mbulula wewe huijui UDOM, Kabla hujapost uwe unachunguza sana!
 
Mkuu uchambuzi wako ni dhaifu sana na umejaa chuki binafsi dhidi ya UDOM, Kama uliomba nafasi hapo wakakupiga chini basi usiwe na kinyongo waache wenzako wasome hapo.
 

Umemaliza kila kitu Kamanda, siongezi neno.
 
Wewe ktk Mambulula wewe ni Mbulularism uliza kwenye sekta mbali mbali wapo akina nani na kutoka chuo gani make
 
ni kweli ila tujue kua mfumo na sheria za hapa chuoni UDOM haziruhusu kabisa masuala ya kisiasa kama tunavyo jua chuo hiki kilijengwa na serikali na kwa sasa ni miongoni mwa vyuo vikuu vinavyo dahiri wanafunzi wengi kuliko vyuo vingine hapa tanzania ila suala la muhimu hapa ni kwamba kuwepo katika siasa inategemeana na intrest za mtu binafsi katika kugombea nafasi fulani ya kisiasa siwezi kusema moja kwa moja kua hawapo kabisa kwani hakuna mwenye ushahidi halisia juu ya hili, kwani tanzania ni kubwa sana kama wabunge hawapo basi madiwani wanaweza. pia tukumbuke kua chuo hiki bado ni kichanga sana kwani kimeanzishwa mwaka 2007 na ni kpindi kimoja tu cha uchaguzi mkuu kimepita tangu kimeanzishwa hivyo ni mapema mno kusema chuo hakizalishi wasomi ambao hatuwaoni katika nyanja za kisiasa. mimi ni mwana UDOM nta gradute 2016, inawezekana 2020 ntaonekana katika majukwaa ya kisiasa nikiomba ridhaa ya watanzania kuwatumikia nikiwa kama msomi kutoka UDOM,,,, tusiwe wepesi wa kubeza jitihada za serikali ambazo ni za kimaendeleo
 

umeandika kisomi sana pamoja sana atuache na udom yetu.
 
Hivi hiki chuo si ndio wanachuo wake uwa wanajipendekza kwa kuwachangia wagombea wa chama fulani kuchukua form?kama sio kujipendekeza ni nini,wao hela zao za nyanya wanategemea ma boom,eti wanajifanya kuchangia wagombea wakachukue form,nadhani UDOM ni category ya vyuo vikuu vya kata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…