Taarabu ni aina ya ngonjera iliyo katika nyimbo. Ndo maana unakuta vikundi mbalimbali vikijibizana katika mada mbalimbali tena kwa lugha ya kimafumbo. Kumbe taarabu kwa yenyewe ilipaswa kuwa na mada mbalimbali kama tulizonazo hapa JF (uchumi, siasa, elimu, lugha, mapenzi, nk). Lakini kwa bahati mbaya watunzi wa nyimbo hizo wamejikita zaidi katika uwanja mmoja: wa mapenzi. Hawana habari na mada zingine.
Kumbe kama ni kuharibu ni hapo kwenye mada. Lingine ni lugha. Wakati mwingine wanatumia lugha kali mno, lugha ya matusi.
Kumbe watunzi wakiweza kupanua wigo wa mada na kutumia lugha ya mafumbo lakini isiyo na ukakasi, naamini muziki huu utakuwa na manufaa makubwa kwa jamii yetu. Sikiliza kwa mfano nyimbo za bibi Kidude ni nzuri sana.