Taarab

Taarab

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Hivi humu JF kuna wapenzi wa Taarab kweli? Mimi napenda sana Taarab aisee. Napenda midundo yake. Napenda jinsi nyimbo zake zilivyo ndefu. Unasikiliza hadi unaridhika.

Napenda jinsi watunzi na waimbaji wake wanavyotumia ujuzi wa lugha kufikisha ujumbe. Hususan napenda jinsi sitiari zinavyotumiwa.

Aah mirindimo ya Taarab swaaafi sana.
 
Unajua taarabu weye? Hebu nitajie kikundi kimojawapo tu cha taarabu!
 
Kwanini umeuliza hapa kwenye mahusiano na mapenzi?Nwy mi sipendi taarabu!
 
sipendi taarab
but napenda tazama wanawake wakicheza taarab....
i hate taarab...
i love taarab....
 
Kwanini umeuliza hapa kwenye mahusiano na mapenzi?Nwy mi sipendi taarabu!

Kwani hapa ni mapenzi kati ya wanaume na wanawake tu? Mapenzi ya vitu na mambo mengine hayaruhusiwi? Mimi ni mpenzi wa Taarab na nimeona niulizie hapa kwenye mahusiano na mapenzi nione kama kuna wengine pia ambao wanapenda. Dhana ya mapenzi ni pana sana.
 
Kwanini mapenzi yanayohusiana na burudani yasiwe kwenye burudani?
 
Kwanini mapenzi yanayohusiana na burudani yasiwe kwenye burudani?

Kwa sababu watawala wa JF hawajakataza wala kuweka bayana ni mapenzi ya aina gani ndo yawekwe hapa.

Soma hii kuhusu jukwaa la MMU:

Tubadilishane mawazo kuhusu mahusiano, mapenzi, urafiki, n.k na kushauriana. TAFADHALI: Hii si sehemu ya kuweka picha chafu ama kutumia lugha kali sana. Zitafutwa!
Kinachokatazwa ni kuweka picha chafu na kutumia lugha kali sana.
 
Mchumu! Mchumu! mchumu! mchumu! mchumu huyo Mwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! I like it
 
Back
Top Bottom