Taarifa: Ambao majina yao hayajaonekana ajira za ualimu

Taarifa: Ambao majina yao hayajaonekana ajira za ualimu

dfreym

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2010
Posts
342
Reaction score
87
TAARIFA!
Nikiwa kama mhanga wa ambao hawajaona majina yao, napenda kusema kwamba, leo nilikwenda Wizarani
na nikaambiwa wahusika hawapo hadi jumatatu, lakini nilifanikiwa kuongea na Naibu Waziri wa elimu ndugu Mlugo na akasema
kwamba yeye hakuwa na taarifa ya kwamba kuna majina hayajatoka ama hayaonekani.

Hivyo akahaidi kufuatilia pia kuonana na wahusika, akaongeza kuwa inawezekana ni errors kwenye computer, akadai kuwa bado walimu 1000 wataajiriwa kwa sababu kuna mahitaji makubwa ya walimu hivyo wote watachukuliwa.

Matatizo hayo hayapo kwa wana UDOM pekee bali vyuo vingine pia, na pia ukitembelea tovuti ya wizara majina ya watu wa shahada hayafunguki kwenye link waliyoiweka.

MWISHO WA TAARIFA.

SOURCE UDOM COLLEGE MATE, 2011.
 
Walimu Ni wito Au Taaluma? Hongereni walimu kwa kuwa na ajira ya moja kwa moja.
 
Poleni mloachwa wadau wenzangu,zaidi tunawaombea ili nanyi mpangiwe kazi haraka iwezekanavyo kama mimi mwenzenu
 
TAARIFA! Nikiwa km mhanga wa ambao hawajaona majina yao,napenda kusema kwamba,leo nilikwenda Wizarani
na nikaambiwa wahucka hawapo hdi j3,bt nilifanikiwa kuongea na N/W wa elimu ndugu Mlugo na akasema
kwamba yy hakuwa na taarifa ya kwamba kn wa2 hawayaoni majina yao,so nilivyomtel akashukuru na kusema
kwamba ndo nimemfumbua macho na anaenda kuonana na wahucka,akasema inawezekana ni errors kwenye computer,
akadai kuwa bdo walimu 1000 wataajiriwa cz kn demand kubwa ya walimu na wote watachukuliwa,
cz matatizo hayo co kwa wana udom hdi vyuo vingine,na pia ukicheki kwenye web ya wizara
majina ya wa2 wa shahada yamefungiwa,hayafunguki,sa cjui ndo wanayaingiza?hyo ni
kwangu so cjui na kwa wengine km ndo yapo hvyo,MWISHO WA TAARIFA.

SOURCE UDOM COLLEGE MATE, 2011.

Uandishi huu ndio unaenda kufundisha watoto wetu,mweee!:shock::shock::shock::hatari:
OTIS
 
hivi mkuu, hapo umeandika kibongo fleva au kifacebook?. hapa jamii forum hatukubaliani na miandiko ya kihuni. asante kwa tarifa. Ova
 
Mhe mwalimu mtarajiwa fasihi andishi yako ni ZERO! Fasihi simulizi ZERO nyie ndio mnaenda kusababisha shule za serikali zionekane zina fanya madudu.
 
Uandishi huu ndio unaenda kufundisha watoto wetu,mweee!:shock::shock::shock::hatari:
OTIS

Tena usije kushangaa jamaa amepangiwa kufundisha kiswahili sasa hizo "cz" "bt" "so nilivyomtel" sipati picha!

Nadhani sasa hivi kwa wasiokuwa na uwezo wa kuwasomesha watoto wao shule binafsi wawafundishe wenyewe tu majumbani.
 
Uandishi huu ndio unaenda kufundisha watoto wetu,mweee!:shock::shock::shock::hatari:
OTIS

Amekwambia ni Mwalimu wa lugha?., pia angalia mda alopost wenda alikuwa anausingizi.
 
Tena usije kushangaa jamaa amepangiwa kufundisha kiswahili sasa hizo "cz" "bt" "so nilivyomtel" sipati picha!

Nadhani sasa hivi kwa wasiokuwa na uwezo wa kuwasomesha watoto wao shule binafsi wawafundishe wenyewe tu majumbani.

Kwa mwendo huu elimu yetu ipo ICU.

Amekwambia ni Mwalimu wa lugha?., pia angalia mda alopost wenda alikuwa anausingizi.

Sasa imagine anaingia darasani na huo usingizi unaodai anao.
Ni balaa.
OTIS
 
Amekwambia ni Mwalimu wa lugha?., pia angalia mda alopost wenda alikuwa anausingizi.

Hata akam ni mwalimu wa sayansi kimu ni lazima aweze kuandika kiufasaha na kueleweka! inaelekea wewe pia ni mmoja wao! na wengi wenu mnataka kuchaguliwa mnapewa posho za kwenda vituoni halafu mnaingia mitini!
 
Mmmm Malima Malima Godfrey! Acha sanaa kijana toka kwa Frank in Clasmates apa ww tena? Aka mie simo mwenyee umeelewa
 
TAARIFA!
Nikiwa kama mhanga wa ambao hawajaona majina yao, napenda kusema kwamba, leo nilikwenda Wizarani
na nikaambiwa wahusika hawapo hadi jumatatu, lakini nilifanikiwa kuongea na Naibu Waziri wa elimu ndugu Mlugo na akasema
kwamba yeye hakuwa na taarifa ya kwamba kuna majina hayajatoka ama hayaonekani.

Hivyo akahaidi kufuatilia pia kuonana na wahusika, akaongeza kuwa inawezekana ni errors kwenye computer, akadai kuwa bado walimu 1000 wataajiriwa kwa sababu kuna mahitaji makubwa ya walimu hivyo wote watachukuliwa.

Matatizo hayo hayapo kwa wana UDOM pekee bali vyuo vingine pia, na pia ukitembelea tovuti ya wizara majina ya watu wa shahada hayafunguki kwenye link waliyoiweka.

MWISHO WA TAARIFA.

SOURCE UDOM COLLEGE MATE, 2011.
Mleta taarifa,
tumejitahidi kufanya editing ya ujumbe wako. Jitahidi kutotumia sms language unapokuwa kwenye majukwaa aina hii. Onesha weledi, werevu na elimu yako kwa kutumia lugha sahihi na siyo kuchezea lugha.

Ujumbe umefika, hivyo turejee kwenye mada wanaJF.
 
Ualimu ni u-punda sio wito tena.

Kuwa mstaarabu ndugu acha kufananisha binadamu wenzio na punda. Una ndugu,jamaa na marafiki huko ambao wanahitaji walimu ili wapate elimu we wawafananisha na punda. Punda anafanya shughuli shughuli za kipunda tambua hilo.
 
Usitegemee haramu kuwa harari mkuu kwa maana msingi wetu wa elimu upo hoi kwanzia enzi za Mungai na bado kuna shule za kata ukiongezea na vyuo vya kayumba na majina ya kuungaunga kama vile vya english course k/k...sasa tutegemee nini kwa products hizi,na je leo hii tutamlaumu huyu mwalimu tu bila kufikiria kwa undani na alikopitia?bnafsi napata picha moja kwamba ni kwa kiasi gani mfumo wetu wa elimu uko kwenye jeneza na kama tunaelewa basi let us change the course

Kuna mda niliandika hapa jamvini kwamba kinachofanyika hapa Tanzania sasa elimu imetushinda na badala yake tunamjaribu mdudu ujinga na victims wa unyangau huu si kwa huyu wala yule tu,hii ni taifa zima,ni over 80% ya poor Tanzanians
 
Back
Top Bottom