Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Kila mwaka Februari 04 huwa ni siku ya kuadhimisha saratani duniani kwa lengo la kutoa elimu, takwimu na uelewa kuhusu Saratani. Na kwa takwimu za mwaka 2024 zimeonesha kuwa bara la Asia ndo linaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya waangaa wa Saratani ya shingo ya kizazi
SARATANI NI NINI
Miili yetu ina chembechembe hai nyingi ambazo huzaliana, hukua, na kufa kwa mpangalio maalum. Chembechembe hizi zinapobadilika na kuanza kuzaliana na kukua katika utaratibu ambao sio wa kawaida ndio zinasababisha saratani. Chembe chembe za Saratani hufuata mfumo huo usio wa kawaida – zinazaliana haraka zaidi bila mpangilio na kukua kwa haraka zaidi na wakati mwingine kuwa na umbile kubwa zaidi. Chembechembe hizi za saratani zisipodhibitiwa/zisipotibiwa mapema zina uwezo wa kusambaa na kuota sehemu nyingine ya mwili wa mhusikaAINA ZA SARATANI
Saratani ni uvimbe unaojitiokeza mahala popote katika mwili wa binadamu, uvimbe huu hauna maumivu yoyote mwanzoni. Saratani zipo za aina nyingi sana na majina yake hutegemea kiungo kilichougua na aina ya chembechembe hai zilizoshambuliwa
Kiungo chochote chaweza shambuliwa mfano
- Shingo ya mfuko wa kizazi
- Matiti
- Ngozi
- Koo na njia ya chakula Tumbo, utumbo, kongosho, ini
- Kibofu cha mkojo na tezi dume
- Mapafu ,ubongo,macho, mifupa,misuli
- Matezi hasa kwa watoto
- Damu nk
NINI HUSABABISHA SARATANI?
1. Matumizi ya Kemikali
2. Ulaji mbovu
3. Kutofanya mazoezi
4. Kutumia pombe kupita kiasi
5. Uvutaji wa Sigara
- DALILI ZA AWALI
- Kila Saratani huwa na dalili zake kutokana na ilipoanzia
- Mara nyingi saratani haina maumivu mwanzoni na ni ngumu kugundua hasa kamma iko kwa ndani
- Uvumbe sehemu yoyote ya mwili
- Mafindofindo
- Mabadiliko ya haja kubwa au ndogo
- Kidonda ambacho hakiponi
- Damu kutoka bila mpangilio au uchafu usio wa kawaida kutoka sehemu za siri(uke)
- Shida kumeza au kupumua