SI KWELI Taarifa hii imetolewa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

SI KWELI Taarifa hii imetolewa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
AJIRAP21AG2025.jpg
 
Tunachokijua
Taarifa zisizo za kweli zinaweza kusababisha kufanyika kwa utapeli baina ya watu katika jamii hasa wale wasiofahamu uhalisia wa taarifa hizo.

Mfano kumekuwepo na taarifa nyingi zinazosambazwa mtandaoni zikihusisha wanaohitaji kufanya mabadiliko ya majina kwenye vyeti vya kuzaliwa, vitambulisho vya uraia (NIDA), vyeti vya elimu katika ngazi mbalimbali na kuwataka kuchangia kiasi fulani cha fedha au kuwasiliana kupitia mawasiliano binafsi yanayoambatanishwa.

Baadhi ya taarifa hizo zilizowasilishwa katika jukwaa la JamiiCheck zilibainika kuwa hazikutolewa na mamlaka husika bali zilighushiwa na watu wenye nia ovu hasa wakitaka kuwaibia fedha wahitaji wa huduma hizo.

Rejea hapa, hapa na hapa. Jambo la msingi unapokutana na taarifa kama hizo usikurupuke kutekeleza taarifa hiyo inachokuagiza, ihakiki kwanza kama imetolewa na mamlaka husika ili kuepuka kutapeliwa.

Taarifa inayosambazwa Facebook kuanzia Agosti 21, 2025

Katika mtandao wa Facebook ipo taarifa inayosambazwa ikidaiwa kutolewa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma akiwataka wenye changamoto za kuhuisha taarifa za vyeti, NIDA au kubadilisha cheti au vyeti kwenye mfumo Ajira Portal, kuwasiliana kupitia whatsApp: +255 621 741 590, Simu: +255 764 892 095

Uhalisia wa taarifa hiyo.

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani haijatolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kama inavyoonekana.

JamiiCheck imebaini mapungufu kadhaa katika taarifa hiyo yanayoitofautisha dhidi ya taarifa rasmi ambazo hutolewa na Sekretarieti ya ajira.

Sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kutofautiana kwa mwandiko (fonts), matumizi ya mawasiliano binafsi (namba ya simu) tofauti inayotumiwa na sekretarieti hiyo.​
1755766677062-png.3447881
Back
Top Bottom