UZUSHI Taarifa hii inayodaiwa kutolewa na jeshi la Polisi kuhusu DKt. Nchimbi ni ya kweli?

UZUSHI Taarifa hii inayodaiwa kutolewa na jeshi la Polisi kuhusu DKt. Nchimbi ni ya kweli?

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Nimekutana na picha hii huko mitandaoni, je ina ukweli wowote kuwa Nchimbi kauwawa na watu wasiojulikana?
Nchimbie.jpg
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook na Instagramkumekuwa na taarifa inayosambaa kuanzia Septemba 9, 2026 na kudaiwa kuwa imetolewa na jeshi la polisi Tanzania kueleza imethibisha kuwa aliyekuwa Makamu wa Rais Tanzania, Emmanuel Nchimbi amefariki dunia.

Taarifa hiyo ikiwemo iliyowasilishwa na mdau imetumia pia Poster inayoonekana kuwa na utambulisho wa chombo cha habari cha Millard Ayo.

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli na haijatolewa na jeshi la polisi Tanzania kama inavyodaiwa.

Taarifa ina kasoro ikiwemo makosa ya kiuandishi mathalani neno "imedhibitishwa" kwenye kichwa cha Taarifa. Hata hivyo kwa nafasi ya Dkt. Emmanuel Nchimbi tukio kama hilo lingetangazwa na mamlaka za juu zaidi.

Jeshi la Polisi Tanzania kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii imechapisha taarifa kukanusha kwa taarifa hiyo ya uzushi na kueleza kuw ainapaswa kupuuzwa. Pamoja na hayo Poster iliyotumika ikionekana kuwa na utambulisho wa Millard Ayo ni ya kubuni tu na si halisi.
Leta link kutoka kwa hiyo media, hiyo picha hata graphics zake haziendani na hiyo media
 
Back
Top Bottom