Taarifa juu ya Miradi ya Mendeleo iliyotekekezwa awamu ya tano ilijaa upotoshaji mkubwa kwa Wananchi

Taarifa juu ya Miradi ya Mendeleo iliyotekekezwa awamu ya tano ilijaa upotoshaji mkubwa kwa Wananchi

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Wananchi wengi walikuwa hawaambiwi ukweli na uhalisia wa miradi iliyotekelezwa awamu ya tano. Kiasi cha Wananchi kuwa taarifa zisizo sahihi juu ya miradi hiyo huku wengi wakidhania ilikuwa imekamilika kwa 100%.

Mfano ni kweli vituo vya afya 460+ na Hospitali za Wilaya zaidi ya 65 zilijengwa. Lakini kiuhalisia nyingi hazijakamilika. Nyingi zilikuwa hazina watumishi na vifaa tiba hata kama zilikamilika majengo.

Ujenzi wa Sgr Dar to Moro huu ndio umekuwa na upotoshaji mkubwa, maana toka 2019 mpaka leo habari ni hizo hizo tu kuwa umekalilika 95% lakini kiuhalisia bado sana maana huenda hata mwaka huu utaweza kukatika bila kuanza.

Kingine ni juu ya bajeti ya dawa, tuliambiwa kuwa awamu ya tano iliamua kutenga bil 400+ kwq ajili ya manunuzi ya dawa ili wananchi waweze kupata dawa wanapoenda kutibiwa. Lakini wananchi wakienda kutibiwa hata dawa hawapati na wengi huwa wanalipia.

Hivyo ili kutoleta mikanganyiko serikali iwe inatoa takwimu sahihi inapotekeleza miradi ya maendeleo
 
Serikali iwe inatoa taarifa za ukweli sasa kuhusu miradi yake. Ni vigumu sana kuficha taarifa hizo kwa mazingira ya sasa.SGR Tangu 2019 wanasema kipande cha Dar Moro kimekamilika kwa zaidi ya asilimia 75 lakini sasa ni miaka miwili mbeleni wala hakuna dalili ya kuanza kutumika kwa kipande hicho!
 
Tuliaminishwa ATCL inafanya vizuri kumbe ni hasara tupu kwa taifa
Marehemu alitaka tu apate 10% yake kwenye dili la ununuzi

Ilikuja kama NGO hapa Mwanza, na mipesa mirefu mno kwa mamillioni ya EURO. Leo hii hao hao wamo kwenye dhahabu! Bilioni zaidi ya 10 alipewa nanihii ....
 
BAVICHA mnapata wapi mda huo wa umbea.
Kwani kipi kaongea uongo? Tuache siasa siasa za ushabiki maandazi.Hii kitu hata mimi ilifika wakati nilishtuka baada ya kudanganywa TZ imejenga viwanda zaidi ya 400.

Mara ikaja kauli mbiu ya Jafo kulazimisha kila mkoa ujenge viwanda 100. Hivo viwanda viko wapi? Umeviona? Ilifika hatua mashine ya chelehani,Printer na photocopy mashine viliolodheshwa km viwanda. Huu ni zaidi ya uzwa uzwa.
 
Kwani kipi kaongea uongo? Tuache siasa siasa za ushabiki maandazi.Hii kitu hata mimi ilifika wakati nilishtuka baada ya kudanganywa TZ imejenga viwanda zaidi ya 400. Mara ikaja kauli mbiu ya Jafo kulazimisha kila mkoa ujenge viwanda 100. Hivo viwanda viko wapi? Umeviona? Ilifika hatua mashine ya chelehani,Printer na photocopy mashine viliolodheshwa km viwanda. Huu ni zaidi ya uzwa uzwa.
400 Au 8,000...Viwanda Elfu 8,000 !😊😊 Niliwahi uliza hapa Kati ya hivo viwznda 8,000 naomba nismvuwe Mkoa was Singuda vipo vingapi,vinejengwa wapi...hakuna mpiga zumari was Jiwe aliyenijibu!
 
Back
Top Bottom