SI KWELI Taarifa kuhusu kuhusu Zungu kufariki ina ukweli wowote?

SI KWELI Taarifa kuhusu kuhusu Zungu kufariki ina ukweli wowote?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
CC: JamiiCheck
Zungu.jpg
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na taarifa zinazoambatana na grafiki ya baadhi ya vyombo vya habari ikieleza kuwa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Azan Zungu amefariki.

Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umefuatilia na kujirirdhisha kuwa Taarifa hizo ni za uzushi na hazina msingi wowote wa ukweli.

Hakuna chanzo chochote cha habari cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo ukilinganisha na ukubwa wake . Wengi waliotoa taarifa hizo ni vyanzo ama watu binafsi.

Mamlaka zinazohusika ikiwamo tovuti ya bunge pamoja na mitandao yake ya kijamii ikiwemo Instagram haijathibitisha pia kutokea kwa taarifa hizo.

Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa grafiki zilizotumika mathalani ya Millard Ayo si halisi bali ni ya kughushi kwani haijachapishwa na chanzo hicho cha taarifa. Grafiki hiyo pia imetumia aina ya mwandiko tofauti na inayotumiwa na Millard Ayo.

Hata hivyo Machi 24, 2026 kupitia mtandao wao wa Instagram bunge wamechapisha video ikimuonesha spika huyo ikiambatana na ujumbe kuwa:

"Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb) leo Machi 24, 2026 amekagua ukumbi wa Bunge ambao umefanyiwa maboresho ya kuwekewa mfumo wa kisasa wa sauti ikiwa ni maandalizi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 3 wa Bunge la 13 ambao mahususi kwaajili kujadili na kupitisha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 ambao utaanza Machi 31, 2026.

Pia, Mhe. Spika ameongoza kikao cha Tume ya Watumishi wa Bunge kilichojadili na kupitisha makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027."
Back
Top Bottom