Taarifa kuhusu uzinduzi wa huduma ya tiba ya Dialysis Hospitali Kuu ya Jeshi

Taarifa kuhusu uzinduzi wa huduma ya tiba ya Dialysis Hospitali Kuu ya Jeshi

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika jitihada za kuboresha huduma ya Afya linatarajia kuzindua Idara mpya ya huduma ya Tiba ya Dialysis katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo.

Shughuli za uzinduzi huo zinatarajia kufanyika kesho Jumatano tarehe 23 Oktoba, 2019 kwenye Hospitali kuu ya Jeshi Lugalo iliyopo Jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili na nusu (2:30) asubuhi.

Mgeni rasmi katika shughuli hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

JWTZ limealika vyombo vya Habari kwenye hafla hiyo muhimu ili kuuhabarisha umma juu ya huduma hiyo kupatikana Jeshini.
 
big achievement JKT....apa nawaza pia JKT waanzishe "Health Promotion activities -- elimu afyaaaa", hili swala la dialysis ni moja ya matatizo makubwa yakumbayo jamii yetu ya leoo. Kuanzia miaka 40 na kuendelea ...

Pia Non communicable disease (NCDs) tunachangamoto kubwa sana kwa kwa sasa....(bia/vileo+nyama+sukari+ulaji usio na tija+matumizi ya dawa hovyo hovyo+ kutofanya mazoez+.............

all the best
 
Hongera sana kwa hatua mliofikia. Huduma hii kwa sasa inahitajika sana. Nafikiri itasaidia kupunguza msongamano pale Muhimbili na hospitali zinginezo.
 
Back
Top Bottom