Taarifa kutoka mahakamani mkoani Singida katika kesi ya uchochezi inayomkabili mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Itilima, Askofu Mwanamapinduzi

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
Ushahidi katika shauri la kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya ITILIMA mkoani SIMIYU Askofu Machumu Kadutu maarufu kama MWANAMAPINDUZI uliopangwa kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo kutoka Agosti 5 mpaka agosti 7 umefungwa siku ya jana Agosti 06.

Siku ya tarehe 05 Agosti Hakimu hakuwepo Mahakamani hivyo kupelekea kesi hiyo kupelekwa siku ya jana Agosti 06,ambapo mashahidi wanne waliweza kutoa ushahidi wao katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida.

Baada ya mashahidi hao wanne siku ya jana upande wa Jamhuri walifunga ushahidi wao na leo Agosti 07 shauri lilienda kwaajili ya uamuzi mdogo ili kuamua ikiwa kama Mshitakiwa ana kesi ya kujibu au hana kesi ya kujibu,mwishowe Mahakama iliamua ya kwamba Mtuhumiwa ana kesi ya kujibu na baada ya hapo Wakili wa upande wa utetezi alipata muda wa kumuandaa mteja wake yaani Mshitakiwa (Machumu) na baadaye mshitakiwa aliweza kujitetea mbele ya Mahakama na hivyo kufunga ushahidi katika upande wa utetezi/Mshitakiwa.

Hivyo Mahakama imetoa order kwa upande wa utetezi na upande wa Jamhuri kuandaa hoja za mwisho (Final submission) kwa njia ya maandishi na zitakuwa filled/registered tarehe 21, Agosti,2025 na ndiyo siku ambayo kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo kwa mara nyingine tena.

Mwanzo wa kesi hii ilipoanza mwaka jana Upande wa Jamhuri walisema ya kwamba wana mashahidi wapatao 13 lakini mpaka ushahidi ulipofungwa siku ya jana kwa upande wa Jamhuri wameweza kupeleka mashahidi 7 tu,hali ambayo inatengeneza wasiwasi sana juu ya kesi hiyo.

Askofu Mwanamapinduzi anakabiliwa na kesi uchochezi katika maneno yake aliyoyatamka mwaka jana katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA ulioongozwa na Mheshimiwa Tundu Lissu katika mkoa wa Singida. Askofu huyo alitamka maneno ya "WAKIWANANIHII MUWANANIHII" hali iliyopelekea yeye kufunguliwa mashitaka hayo.

Mwanzo wa kesi hii Askofu huyo alikuwa akisimamiwa na Wakili wake TUNDU ANTIPAS LISSU lakini kwa siku za hivi karibuni amesimamiwa na Wakili HEMED KULUNGU pamoja na Wakili Hekima Mwasipu ambao hawa wote wanamuwakilisha Wakili Tundu Lissu ambaye yupo kizuizini.

Haki huinua Taifa.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…