Taarifa kwa umma, ajali ya treni ya mjini kwenda Pugu

Tanzania Railways Corp

Govt Institution
Joined
Mar 23, 2018
Posts
292
Reaction score
690
f14b30bc-6a19-4dc2-84fc-21169ecf80c3.jpeg

Pia soma ~ Ajali ya Treni ya Dar maeneo ya Karume, mabehewa yameacha njia

TAARIFA KWA UMMA AJALI YA TRENI YA MJINI KWENDA PUGU
​
Dar es Salaam, Mei 13, 2025.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linauarifu umma kuwa leo Mei 13, 2025 treni ya mjini kwenda Pugu, iliyotoka Stesheni ya KAMATA majira ya saa 10:00 jioni kuelekea Pugu Jijini Dar es Salaam, imepata ajali kwenye makutano ya reli na barabara ya Kawawa majira ya saa 10:05 jioni.

Kufuatia ajali hiyo iliyohusisha mabehewa 12 yaliyobeba abiria takribani 1,200, wataalamu wa Shirika pamoja na timu ya afya ya Shirika, walifika na kutoa msaada wa huduma ya kwanza ambapo majeruhi kumi wakiwemo wawili wanaume na nane wanawake, wamekimbizwa hospitali ya Rufaa ya Amana kwa matibabu zaidi.

Chanzo cha ajali hiyo ambayo imesababisha mabehewa 6 kuathirika bado hakijafahamika na Shirika litatoa taarifa zaidi.

Kufuatia ajali hiyo Shirika linauarifu umma huduma ya usafiri wa treni ya mjini kwenda Pugu, utaendelea kesho kama kawaida

TRC inatoa pole kwa kila mmoja aliyeathirika na ajali hii kwa namna moja ama nyingine.​

Fredy Mwanjala
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano
 
mtuelezi vizuri ni treni ya kigoma au SGRA maana mnajua watu wanao opanda ndege mpaka waage mlivyo wapuuzi CCM
 
NAANGALIA EATV
NAONA AJALI YA TRENI

MABEHEWA YAMEHAMA NJIA

KWA WANAOJUA MTUPE UPDATES JAMANI

MM LIKE TRENI NINALIOANAGA PALE RELINI NIKIWA NA KUNYWA KA BIA KANGU OPP KWA KWELI NILIAPA SITOKAA NIPANDE KAMWEE

YAAN UKIANGALIA TU YALE MABEHEWA N SHIDA SAA YOYOTE YANADONDOKA

HAHAHA NDUGU YANGU JOSEPH KAMA UMESIKIA HAYA KUMBUKA NILIKUONYA

MUNGU AWAPE WEPESI WOTE WALIOUMIA NA KUFARIKI
KAMA WAPO
 
Pia soma ~ Ajali ya Treni ya Dar maeneo ya Karume, mabehewa yameacha njia

TAARIFA KWA UMMA AJALI YA TRENI YA MJINI KWENDA PUGU
​
Dar es Salaam, Mei 13, 2025.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linauarifu umma kuwa leo Mei 13, 2025 treni ya mjini kwenda Pugu, iliyotoka Stesheni ya KAMATA majira ya saa 10:00 jioni kuelekea Pugu Jijini Dar es Salaam, imepata ajali kwenye makutano ya reli na barabara ya Kawawa majira ya saa 10:05 jioni.

Kufuatia ajali hiyo iliyohusisha mabehewa 12 yaliyobeba abiria takribani 1,200, wataalamu wa Shirika pamoja na timu ya afya ya Shirika, walifika na kutoa msaada wa huduma ya kwanza ambapo majeruhi kumi wakiwemo wawili wanaume na nane wanawake, wamekimbizwa hospitali ya Rufaa ya Amana kwa matibabu zaidi.

Chanzo cha ajali hiyo ambayo imesababisha mabehewa 6 kuathirika bado hakijafahamika na Shirika litatoa taarifa zaidi.

Kufuatia ajali hiyo Shirika linauarifu umma huduma ya usafiri wa treni ya mjini kwenda Pugu, utaendelea kesho kama kawaida

TRC inatoa pole kwa kila mmoja aliyeathirika na ajali hii kwa namna moja ama nyingine.​

Fredy Mwanjala
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano
Hii SGR bila kubinafsishwa ni uongo na watapaki mabehewa yote mahali.
 
Treni ya mwakyembe,hiyooo
Usafiri wa walalahoi.....inajaza
Ngombe wenyewe wanasubiri
Nasikia humo ndani nusu ya abiria ni vibaka 😄

Ova
 
Kiongozi ilitakiwa ujue chanzo cha ajali ndio kesho safari iendelee kama kawaida kutangaza safari ipo bila kujali nini sababu ya ajali ya jana mnaonekana mnafanya kazi chini ya kiwango..
 
Back
Top Bottom