Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuhusu zoezi la maboresho ya mfumo wa mita za Luku ambapo sasa ni zamu ya mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.
Zoezi hilo litaanza kufanyika katika mikoa hiyo kuanzia tarehe 26 Agosti 2024. Maboresho haya yanalenga kuendana na viwango vya mifumo ya LUKU vya kimataifa na kuongeza ufanisi na usalama wa mita za LUKU nchini.
Mteja atakaponunua umeme kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe tajwa atapokea tarakimu kwenye makundi matatu, kila kundi likiwa na tarakimu ishirini. Kundi la kwanza na la pili la tarakimu yatakuwa kwa ajili ya maboresho na kundi la tatu la tarakimu litakuwa ni la umeme ulionunuliwa.
Mteja ataingiza tarakimu za kila kundi kwa kufuata mpangilio unaosomeka kwenye risiti ya malipo au ujumbe mfupi wa simu (sms) na kila atakapoingiza kundi moja Mteja atapaswa kubonyeza alama ya kukubali ya # au mshale wa kukubali na hapo atakuwa amefanikiwa kuboresha mita yake na kupokea kiwango cha umeme alichonunua.
Zoezi hili ni bure na litafanyika mara moja tu kwa mteja, baada ya kufanya hivyo mteja atakuwa amefanya maboresho hayo na ataendelea kupata kundi moja la tarakimu ishirini kila anapofanya manunuzi ya umeme.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya huduma kwa wateja 0748 550 000 au namba za huduma kwa wateja mikoa husika au WhatsApp 0748 550 000 na mitandao yetu ya kijamii.
Shirika linawahimiza wateja wake wote kuendelea kununua umeme ili kuweza kufanya maboresho hayo kwenye mita zao ambapo ukomo wa zoezi hili katika maeneo yote nchi nzima utakuwa tarehe 24/11/2024.
Imetolewa Na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA
TANESCO - MAKAO MAKUU
DODOMA
TANESCO: MITA YAKO TUNA KAZI NAYO
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Irene Gowelle akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mha Gissima Nyamo-Hanga kutoa taarifa ya zoezi la Maboresho ya mfumo wa LUKU kwa wateja wa Kanda ya Kati na Kaskazini ambapo zoezi hilo litaanza rasmi kwenye mikoa hiyo tarehe 26 Agosti, 2024.
Pia, soma: Maboresho ya mita za luku kwa wateja wa kanda ya kati na kanda ya kaskazini