University of Dodoma (UDOM)
Public Institution
- Feb 24, 2024
- 50
- 55
Chuo kinapenda kuufahamisha umma kuwa, kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa, mwanafunzi anayestahili kurejeshewa fedha huwasilisha madai yake rasmi. Baada ya kupokelewa, madai hayo hufanyiwa uhakiki na ofisi inayohusika na malipo ya ada kwa kulinganisha taarifa na kumbukumbu za mwanafunzi, kabla ya malipo kuidhinishwa na kufanyika.
Utaratibu huu wa uhakiki ni muhimu ili kuhakikisha kuwa marejesho yanafanyika kwa usahihi na kwa kuzingatia taratibu za kifedha za Chuo. Utaratibu wa uhakiki unapokamilika mwanafunzi anarejeshewa fedha yake.
UDOM inapenda kuwahakikishia wanafunzi na umma kwa ujumla kuwa tayari wanafunzi wenye viambatanisho stahiki wamerejeshewa fedha zao na kwamba, zoezi la uhakiki na urejeshwaji wa fedha hizo linaendelea.
UDOM inawaomba wanafunzi husika kuwa na subira wakati hatua za mwisho za uhakiki zinakamilishwa. Aidha, mwanafunzi mwenye changamoto yoyote anashauriwa kuwasiliana na uongozi ili kutatua changamoto yake kwa wakati.
Uongozi wa UDOM unathamini maoni na mrejesho wa wanafunzi na wadau wake na unawahakikishia kuwa madai yenye sifa na yaliyothibitishwa yatafanyiwa marejesho kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
UDOM inaendelea kujizatiti katika kulinda ubora wa elimu na ustawi wa wanafunzi wake.
Imetolewa na:
Beatrice BaltazaryKaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
Soma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) turejesheeni malipo yetu ya Ada yaliyozidi, mnatuzungusha kila siku