Polisi mkoani Arusha imekamilisha 9uchunguzi wake kuhusiana na kuungua kwa ofisi za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kusema wanachama wa Chama hicho ndio waliohusika.
hata hivyo, Mbunge wa Arusha Mjini (chadema) Godbless Lema amepinga kauli hiyo na kulipa jeshi hilo siku nne kuwakamata na kuwahoji watuhumiwa watano baada ya kulipatia majina hayo akidai kuwa ndio wanaohusika na uchomaji moto ofisi za chama hicho.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Japhet Lusinga alisema;
".. katika uchunguzi wetu tumebaini kuwa hakuna mahali palipovunjwa kutoka nje ya uzio na kuruhusu watu kuingia ndani...tumegundua kuna tundu dogo darini eneo la kuelekea bafuni la upana wa futi moja na nusu kiasi haliwezi kuruhusu mtu kupita.
Tumejiridhisha kuwa hakuna mtu anayeweza kupita hapo na ndani tulikuta majibu na baadhi ya vitu vilivyoungua na vifaa vingine.."
SOURCE:
Mwananchi, alhamis, desemba 5, 2013 (FRONT PAGE)
MY TAKE:
Polisi watuambie ripoti ya uchunguzi wa mlipuko wa bomu imefikia wapi.,maana kama hali iko hivi nina mashaka kuwa hata mlipuko wa bomu inawezekana waliutengeneza wenyewe kama zilivyo hisia za wengi katika watu wenye kuwaza sawasawa.