Taarifa maalumu, 'operation' imesitishwa, nuru imeonekana na 'the State' wamesema apewe muda

Taarifa maalumu, 'operation' imesitishwa, nuru imeonekana na 'the State' wamesema apewe muda

duuu hili jamaa,ona sasa.Mi nafikiri inaezekana kuna kitu jamaa yupo nacho au basi ndo walee(wasojulikana)
Lakini la kukopa kopa naona bado hajasikia,twambie 'mtafanya nini sasa??
 
Operesheni imesitishwa hadi lini? maana tupo tumekata almost 70% ya mwaka "ujao" na hamna dalili yoyote!
 
Nimekusoma mkuu

Changamoto ya kwanza ni katiba. Rais anapata madaraka yake kwenye katiba ambapo 'theState', pamoja na kuwa na capacity, wako well trained kujua mipaka yao, kwamba lazima katiba na sheria ziheshimiwe.

Ikiwa sisi tutaona ni sawa kuvunja katiba na kuyapoka madaraka ya rais, basi nasi hatutakuwa tofauti na hao tutakaokuwa tunataka kuwapoka madaraka. Lazima kila mtu afanye kazi kwenye misingi ya utawala wa sheria.

Ajenda kuu na ya mwanzo kwa sasa, hasa kuanzia kipindi kile cha awamu ya nne na yaliyotokea awamu ya tano, ni uundwaji wa katiba mpya. Sasa imekuwa lazima na pressure imekuwa kubwa sana hata pale 'stpeters'.

Kwa miaka mingi 'stpeters' pale kumekuwa na nguvu kubwa kwenye kulinda wakubwa. Lakini sasa kwa madhaifu ya nyuma na matatizo ya hapa karibuni, wapo wanaoona umuhimu wa kuwa na taasisi zitakazofuata msingi ya sheria na haki.

Kumbuka 'stpeters' na 'theState' sio taasisi moja. Hawa 'theState' wao wametoa muda mpaka mwakani kwa mchakato wa katiba kuanza. Nachelea kusema kama 'aliyepewa muda' hataanza hili inaweza kuwa 'too late' kwake.

Sasa kule 'stpeters' bado kuna wale conservatives ambao wanataka mambo yaende hivihivi na wanaamini wanazo means za kuhakikisha inabaki hivi. Wapo ambao wanashughulikiwa kimyakimya na muda mchache hawatakuwepo tena. Watakaobaki wakiendelea wanaweza kufanya too late ya 'aliyepewa muda' isiwe beyond mwakani.

Traditionally, kwenye miradi huko na utendaji kuliachiwa wanasiasa. Maslahi ya kiuchumi yaliachwa sana kwa watendaji serikalini. Mabadiliko ya kuweza kuwa na 'economic intelligence' kwenye taasisi ya pale 'stpeters' yatakuja mfumo wote utakapobadilishwa.

Yaani hii itakuwa transformation kubwa sana kuona focus isiwe tu kwenye ulinzi na usalama bali iende pia kwenye uchumi na biashara. Hapa bado kuna jukumu kubwa sana ila najua wapo watu kadhaa pale 'stpeters' wamekuwa wakipikwa kwa takribani miaka 12 sasa. Mmoja wao akipewa kuongoza ile idara basi anaweza kuleta tija.

Mpaka wakati huu hakujakuwa na vitendo vya kulipiza kisasi. Watu wamebadilishwa na wengi wamepewa nafasi nyingine, tena zenye heshima kabisa, ili wapate nafasi ya kujitafakari na kujipanga. Ila utashi wa kisiasa utaamua nani abaki na nani aendelee.
Mkuu

The state wameridhishwa na kikosi kazi cha mkandala!?au ni janja janja ya Aliyepewa muda ku delay mchakato HALISI Hadi 2025 uchaguzi Ili washinde KWA katiba iliyopo!!?


"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!
 
Imeamuliwa 'next stage' isitishwe. Baadhi ya maombi ya unyenyekevu ya 'theState':

1. Sheria zifuatwe na zile zisizofaa zibadilishwe.
2. Mwakani kuwe na mwendelezo wa kuandika katiba ambapo bunge liundwe na lisilazimike kuingiza wabunge waliopo sasa isipokuwa wale wenye tija.
3. Wabunge wasiokuwa halali waondolewe kutoka bungeni.
4. Ikiwezekana yale majimbo na kata ambayo ilionekana kabisa kulikuwa na upotoshaji wa matokeo basi uchaguzi urudiwe. Uchaguzi wa serikali za mitaa usubirie mpaka katiba mpya.
5. Stahiki za wafanyakazi wa umma na wastaafu zilipwe. Fao la kujitoa lirejeshwe kwa wale waliopoteza ajira.
6. Fungua milango ya nchi ili biashara na mitaji ikaribie na ku-unlock uchumi. Wawekezaji wakaribishwe kwa sera na sheria wezeshi.
7. Wananchi kule kimara walipwe fidia na kwingineko ambapo watu waliumizwa.
8. Ofisi ya DPP na mwanasheria mkuu ifumuliwe na watu watendewe haki.
9. Watendaji wote 'walio-dance the tune' na kuvunja sheria huku wakiumiza watu waondolewe.
10. Miradi ya SGR na Stiegler's iendelezwe pamoja na ile ya barabara lakini upembuzi ufanyike ili ikiwepo isiyo na tija iachwe.
11. Kuna tatizo kubwa sana deni la taifa.. angalau punguza sasa kukopa na weka mazingira ili uvutie wawekezaji na hasa wale wa ndani ambao wameficha matrilioni ardhini na nje ya nchi.
12. Uchunguzi huru ufanyike kwa yale matukio yote ya utekaji, mauaji na mashambulizi dhidi ya binadamu.
13. Ondoa elimu bure kwasababu inajenga taifa lenye 'irresponsible' minds. Angalia namna ya kubadilisha mfumo wa elimu ili uendane na nyakati tulizonazo.
14. Fanya maridhiano na wapinzani na taasisi zilizotengwa ili kuleta umoja wa kitaifa.
15. Serikali iendelee kubaki Dodoma na ikiwezekana ikulu ya Dar es salaam pajengwe kituo maalum cha utalii.
16. Chama bado kina misingi mizuri, imarisha kwa kuteua watu wenye maono na uzalendo kwa nchi.
17. Sisi hatutakuja kukuingilia, teua na unda timu kwa kadri unavyoona inafaa.. watendee watu haki nasi tutaendelea kukuunga mkono.

18. Mpaka sasa umetuonesha mwanga mwema nasi kwakuwa tunaipenda nchi tumesitisha 'mipango' yetu ili utimize majukumu yako na kusimamia haki.

Tulishauri, hakusikiliza na sasa hayupo. Nimepewa ujumbe, nimeufikisha.
Huu uzi mbona bado hatuoni Future? TA alituingizachaka?
 
Jambo unalopaswa kujua ni kwamba 'hatma' ipo kwenye ule ujumbe wa rais ambaye hajawahi kugombea ila fursa ya 'neema' inaachiliwa kufanya remedy.

Hakuna maono ambayo hayapo subject to changes. Ikiwa tu zile condition zilizopelekea maono zitabadilika basi maono pia yaweza kubadilika.

Madam president kaonesha tofauti na hapa anapatiwa nafasi ya kufanya namna inayobadilisha maono.

Asipofanya ile dhamira ya awali inakuwa na uhalali kuendelea.
Kwa hiyo ndio maana mmemuacha aanze kufanya mikutano ya kampeni za 2025 Sio!?

Kwamba anafuata vizuri maelekezo yenu si Ndio!?
Mbona ishu ya katiba kama anachenga hivi,halafu elimu hajabadili mitaala zaidi anacheza dana dana au!!

Demokrasia ya mikutano haipo tena Mbona au we unaona sawa sio!!?

Tryagain NJOO ujibu na huku!!!
 
Back
Top Bottom