Kama Samia amejitokeza kugharamia matibabu ya Sativa aachwe afanye hivyo, watu wa X wapunguze ujuaji kutegemea michango ambayo hawajui itapatikana kiasi gani, na kwa muda gani, huku mgonjwa akiwa hospitali, wawe makini, watumie na akili.
- Samia kugharamia matibabu ya Sativa ni kodi zetu, ni haki yetu, lakini pia ni jukumu lake akiwa kama chief comforter wetu, aachwe afanye hivyo bila kelele.
Hii issue inahitaji organisation, sio mihemko; kuendelea kuikumbatia watu wa X pekee haitaleta majibu, zaidi itasababisha chuki izidi kukua kwenye jamii yetu.
Hapa tukubaliane au tukatae, Samia ndie kiunganishi wetu kwenye hili suala, kauli yake moja tu ya kukemea utekaji na uteswaji itamaliza kila kitu, aambiwe afanye hivyo akiwa pia anaendelea kusaidia matibabu kwa mgonjwa.
Kuendelea kumchangia Sativa huku tukiendelea kuishi kwenye jamii yenye chuki, itakuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
- Samia anatuchukia? If not, kwanini yupo kimya mpaka leo?
Tutaendelea kutekwa na kuteswa, na wakati mwingine kuuwawa, watawala wao hawatakuwa na hasara yoyote, sisi, familia zetu, na marafiki zetu ndio tutakaoumizwa, akili na busara vitumike.