Maneno mengi, ufafanuzi mrefu, the guilt are afraid, hivi ulitegemea daktari wa rais aseme nini?. Hii ni kazi ya Salva, kisa Mwanahalisi kaibua mashaka.
Jamani tangu tumepata uhuru, hii ndio mara yangu ya kwanza kuona taarifa ya hali ya rais ikiwekwa hadharani. Taarifa hiyo ni ya kweli but the man is also sick.Urefu wa taarifa hii unatia shaka kuwa kuna jambo linataka kufunikwa. Inanikumbusha siku ile ya uzinduzi upimaji wa hiari, Mzee Mengi alipopima tuu pale Angaza ya Amref, akatoka nje na kuonyesha cheti kuwa yuko salama.Wadadisi wa mambo wakawauliza Angaza, hivi mnatoa cheti kueleza fulani yuko salama, au majibu ni siri, wakajibu majibu ni siri na huwa hawatoi cheti, ila kwa vile mzee ni public figure, wametoa ili kuhamasisha upimaji.
Kitu ambacho kinajulikana, ukipima, unapewa majibu yako kwa siri, ila unauhuru wa kujitangaza hadharani kama unao au hauna na sio hii ya kupeana vyeti.
Hii taarifa ndefu ya daktari wa Ikulu ya nini lakini?! Liko jambo and time will tell. Cha muhimu tumuombee rais wetu, afya njema, angalau amalize salama 2010 tena madaktari msisitizieni apumzike baada ya 2010 ili kuilinda afya yake mgogoro, vinginevyo...
Get well Soon Mr. Presidaa and by the way sikupata nafasi jana, "Happy Birth Day"