Sasa imewekwa wazi, na wananchi wameondolewa wasiwasi kuwa Rais wao ni mgonjwa baada ya kuwa anazidiwa mara kadhaa kila anapopatwa na kile kinachoelezwa kuwa uchovu wa kazi.
Leo Daktari wa Rais Jakaya Kikwete, Peter Mfisi ameibuka na kuqweka kila kitu hadharani kuhusu afya ya Rais wetu.
Daktari huyo akiwa Ikulu, akasema Rais Kikwete hana Ukimwi, hana kansa, hana dalili za kiharusi na kamwe hakuna kaugonjwa kokote kwenye damu yake wala nyama zake.
Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Rais Kikwete kuishiwa nguvu wakati akihutubia katika Jubilee ya miaka 100 ya Kanisa la Africa Inland Tanzania (AICT) jijini Mwanza wiki iliyopita.
"Naelewa fika kutokana na kiapo cha udaktari na maadili yangu, siruhusiwi kutoa hadharani undani wa habari yoyote inayohusu mgonjwa ninayemtibu bila ridhaa yake...
... Kwa kuwa huyu ni Rais wa nchi, na suala la afya yake ni kwa maslahi ya Taifa na umma wa Watanzania kwa ujumla, na kwa kuwa yeye ameridhia kutolewa kwa habari za afya yake ili watu wajue ukweli na kuondoa hofu, nimeamua kufanya hivyo,"alisema Mfisi.
Alisema kila mara Kikwete amekuwa akipimwa na kufanyiwa uchunguzi wa afya yake na madaktari wa Tanzania na wale wa nje ambako huenda mara kwa mara na wote wamebaini kuwa hana kaugonjwa kokote kanakowez kufikiriwa na yeyote.
Mungu Mkubwa jamani, yote mabaya yaliyokuwa yakielezwa na wale wachokozi, kumbe hamna kitu na hiyo imethibitishwa na madaktari wake na wale wa nje, ambao nasikia hawana punje ya rushwa hata kusema uongo.