Taarifa ya JWTZ kwa Umma

Taarifa ya JWTZ kwa Umma

Status
Not open for further replies.
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM,12Septemba, 2013.
Tele Fax : 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz

Taarifa kwa vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limepata habari kupitia mtandao wa Jamii Forum na Gumzo la Jiji na mingineyo kuwa likizo zimesitishwa Jeshini na waliokuwa likizo wameitwa kurudi kazini.

Taarifa hizo pia zimeeleza kwamba Brigedi za Tembo na Kifaru zimepewa maagizo ya kuwa katika hali ya utayari endapo watahitajika kusonga mbele.

JWTZ linapenda kuwaeleza wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji mtupu na hazina ukweli wowote. Aidha, taarifa hizo ni zenye nia ya kuzorotesha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu (Tanzania) na majirani zake.

Sambamba na taarifa hii, pia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa za kutohusika na viunganishi vya JWTZ kwenye mitandao ya ‘Facebook‘ – (Facebook/JWTZ) na ‘Twitter‘ (Twitter/ JWTZ). Mitandao hiyo yenye viunganishi vya JWTZ imekuwa ikijihusisha na kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikichangiwa na watu mbalimbali, ambapo baadhi yao wamekuwa wakitoa taarifa za upotoshaji na zisizo sahihi. Tunapenda kutaarifu kwamba akaunti za facebook na twitter zilizotajwa siyo za JWTZ.Hatua zimechukuliwa za kuwatambua wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.




Aidha inasisitizwa kwamba JWTZ lina taratibu za zake zinazotumika kufanya mawasiliano na Vyombo vya Habari, Taasisi, au mtu binafsi kuhusu utoaji wa taarifa. Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi
Dar es salaam, Tanzania
 
mikwara ya nini...kama ni uongo wakanushe sio kutapatapa kwa mikwara.
 
Hiyo email address ya JWTZ ni kichekesho namba moja.
Kichekesho namba mbili ni hiyo website.....HAIPO.
 
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : "N G O M E" Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM,12Septemba, 2013.
Tele Fax : 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz

Taarifa kwa vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limepata habari kupitia mtandao wa Jamii Forum na Gumzo la Jiji na mingineyo kuwa likizo zimesitishwa Jeshini na waliokuwa likizo wameitwa kurudi kazini.

Taarifa hizo pia zimeeleza kwamba Brigedi za Tembo na Kifaru zimepewa maagizo ya kuwa katika hali ya utayari endapo watahitajika kusonga mbele.

JWTZ linapenda kuwaeleza wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji mtupu na hazina ukweli wowote. Aidha, taarifa hizo ni zenye nia ya kuzorotesha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu (Tanzania) na majirani zake.

Sambamba na taarifa hii, pia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa za kutohusika na viunganishi vya JWTZ kwenye mitandao ya ‘Facebook‘ – (Facebook/JWTZ) na ‘Twitter‘ (Twitter/ JWTZ).Mitandao hiyo yenye viunganishi vya JWTZ imekuwa ikijihusisha na kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikichangiwa na watu mbalimbali, ambapo baadhi yao wamekuwa wakitoa taarifa za upotoshaji na zisizo sahihi. Tunapenda kutaarifu kwamba akaunti za facebook na twitter zilizotajwa siyo za JWTZ.Hatua zimechukuliwa za kuwatambua wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.



Aidha inasisitizwa kwamba JWTZ lina taratibu za zake zinazotumika kufanya mawasiliano na Vyombo vya Habari, Taasisi, au mtu binafsi kuhusu utoaji wa taarifa.Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi
Dar es salaam, Tanzania

Mleta uzi na gazeti lako mnatuchanganya..
Mbona hii taarifa haioneshi kuilaumu JF au kuichukulia hatua yoyote??
 
Huu ni mkakati wa gazeti la Jamboleo kuogofya JF great thinkers ambao wamemkomalia mmiliki wake na Biashara ya Bwimbwi a.k.a Ubuyu a.k.a Poda a.k.a Sembe.
Yaani JWTZ watoe tamko kupitia hili gazeti la udaku ??????????????
 
wanaweza kufuatilia na kuwatia nguvuni wote wanao chochea chuki kati ya tz na rw,ni rahisi kabisa ila ambacho sina uhakika nacho ni wanauwezo na technology hiyo?na kama kweli ile account ya twitter ni ya kwao basi watakuwa wamewaonea watu maana details zilizonyingi nimeziona kwenye tweet zao...
Ni kazi yao kuzuia uchochezi maana uchochezi ni chanzo cha uvunjifu wa amani ...na kikiishanuka wao ndo wataambiwa waende vitani na siyo wana JF...hivo kuweni makini mnapotumia vidole vyenu
 
watu wengine wanapenda kutunga uongo ndiyo zao wanafanya jf ionekane mtandao wa kuzua uongo kumbe wao ndiyo waongo na wazushi wakubwa.
 
Watawachukulia hatua jf? Nijuavyo mimi jf=Watanzania, hii ina maana kua habari zinazopatikana jf huandikwa na wanachama wa jf ambao wengi wao ni Watanzania. Sidhani kama wasimamizi wa jf huwatuma watu kuandika habari yeyote, wao kazi yao ni kuchuja habari kama ni za ukweli ama za uzushi na kuzifuta.
Kwa mtazamo huu jwtz wanataka kupambana na Watanzania, sawa tusubiri ila wakati wanafanya hivyo wasisahau kusoma "disclaimer" ya jf waone inasemaje ndipo waje na mikakati yao.

JWTZ, ni member hapa JF? Nisaidieni
 
Wadau nawasalimu woote,,
Leo asbh kupitia vpindi vya MAGAZETI redioni zimeskika habari kuwa Jeshi la Wanachi Tz limetangaza mgogoro usiokoma kati yake na mitandao ya kijamii ikiwemo JF kwa kile kibachodaiwa kuwa Wamepakaza habari za uwongo kuwa Likizo zoote kwa Wanajeshi zimefutwa na wanajesh walokuwa likizo kurejeshwa makazini mara moja kufuatia hali ya hatari iliyokuwa imetanda nchini, JWTZ imedai kuwa habari hizo ni za kipotoshaji na uongo mkubwa na serikali haitasita kuwachukulia hayua wahusila.

Anaejua undani wa hili afunguke hapa

Shule za kata bwana wewe kwanini ukimbilie kupost habari ambayo huna data huu uzi kunamtu kapost subiri mods wakusaidie kuunganisha na uzi ulokwenda shule sawa
 
Hiyo email address ya JWTZ ni kichekesho namba moja.
Kichekesho namba mbili ni hiyo website.....HAIPO.

Usikute hapo kuna raia walishavuta mpunga wa kutengenezwa site...

Halafu taasisi kama Jeshi inatumia public/global mailing system....kazi ipo ten si ndogo!!!
 
Hawa Viongozi wetu wa JWTZ wanataka kuanza kutisha watu mbona matukio mengi tu hawajayatolea ufafanuzi ili kujisafisha?
1. Tumeshuhudia Magari na wanajeshi wakikamatwa na Meno ya Tembo wamechukua hatua gani hadi sasa?
2. Tumeshuhudia baadhi ya wanajeshi wakijihusisha na ujambazi wamechukua hatua gani?
3. Wanajeshi wanatajwa kuhusika kuteka, kutesa, kuiba mali za raia pamoja na kubaka kule Mtwara wamechukua hatua gani?
4. Shimbo anahusishwa na kupora fedha za wanajeshi waliokuwa wakitumikia UN na kuzificha Uswiss je wamechukua hatua gani?
5. Nchi hii sasa biashara ya Madawa ya kulevya imeshamili katika nchi hii na wao wamekula kiapoa cha kuilinda Tanzania wananchi na Mipaka yake je wamechukua hatua gani kwani tatizo bado ni kubwa.
6. Je na yale mazoezi waliyoyafanya hivi karibuni ambayo walisema ni ya kujiweka tayari na kujenga ukakamavu yalikuwa na lengo gani?

Mimi nafikiri wangejikita kwenye matatizo hasa yanayoikabili nchi hii kuliko kujiingiza kwenye kujibu mambo ya humu JF ambayo hayatalisaidia taifa hili
 
Hahahahaa....na mimi nasema apigwe tu.

lazima tukubaliane,nchi inaendeshwa kwa kanuni...sasa yeye anajifanya hodari ..watampiga...na mimi nasema apigwe tuu..maana wamechoka
 
Sawa nimekuelewa kwamba inawezekana kupata IP address kwa kadri inavyotakikana. Na kwa mwendo wa humu jf tutasombwa wengi sana.

Bado kabisa huwezi kum track mtu kwa kutumia IP address hapo tanzania due to our local address wewe unakaa tandale hata gprs haisomi hiyo location ataona wapi hebu www.myipaddress.com nitumie ip addrees yako nijaribu ku track nikwambie ulipo na wewe mwenyewe utatoa jibu sawa
 
yasije yakawa kama ya misri ya kufungia facebook kisa chanzo cha vurugu, na watataka kuifungia jf pia.
 
Mimi nilisema, JAMANI HAYA MAMBO TUNAYOZUNGUMZIA SIYO YA NDANI SANA AMBAYO HAYATAKIWI KUWA PUBLIC? Majibu niliyopata ikabidi ninyamaze tu, na waliokuwa wakifunguka ni watu prominent sana hapa JF na kwenye media zingine! Tena walijitetea kabisa kuwa data za ndani hawajazitoa (kwa maana hiyo wana data za ndani pia!!!). Naona kuna tatizo kubwa sana kwa majeshi yetu yote, kuanzia ulinzi mpaka usalama! Itakuwaje watoe siri za Jeshi kwa wanahabari, ILI IWEJE? Maadili yameporomoka tu sana, leo hii adui anaweza kupeleleza chochote hata bila kuja Tanzania, anaingia JF tu na kuanza kuwachokonoa watu wanafunguka! Kua uzi mmoja uliwahi kuwapo humu nadhani ni 2008 au 2010, Ulikuwa unatoa habari za ndani sana za JW, mpaka siraha zilizopo kwenye vikosi mbalimbali na nyingine zisizotakiwa kujulikana, nadhani uzi huo baadaye modes waliona wakaufunga! Tuchunge midomo yetu jamani tunajiuwa wenyewe!!
 
Ndiyo hawa jamaa katika zama hizi, kwenye maazimisho ya sherehe zao huwa wanavunja mawe na matofali kwa vichwa?

Jwtz should upgrade their software at least to windows 98 bana,stil wapo dos,

Wajifunze si kila kitu ni kibaya kikisemwa juu yao,
Mbona wanahosti email yahoooo!!!!!too much physical
 
tehetehetehet dah JF sio mtu mmoja kama kubenea jamani. \wala founders hawaanzishi threads hapa. Tunaanzisha thread sisi na kutoa sources of the habaris
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom