TAARIFA YA KURUDIWA KWA WRITTEN PRACTICAL ASSESSMENT (WPA)
ILIYOFANYWA NA KUNDI LA 42 NA KUNDI LA 40 WALIOFANYA MARUDIO
(SUPPLIMENTARY) TAREHE 18-26 JUNI, 2026
Taarifa inatolewa kwa wanafunzi wa Kundi la 42 na watahiniwa wa Kundi la 40 waliofanya mitihani ya marudio (supplementary) kuwa; katika kikao chake Maalum kilichofanyika tarehe 6 Julai, 2026, Bodi ya Uendeshaji ya Taasisi imeamuru kurudiwa kwa Written Practical Assessments (WPA's) zilizofanyika tarehe 18-26 Juni, 2026 baada ya kubainika kwa udanganyifu uliofanywa wakati wa ufanyikaji wa WPA's hizo.
Marudio ya WPA yatafanyika_katika muda utakaopangwa na Taasisi baada ya kukamilika kwa Mafunzo ya Uwandani (field placement) kwa Kundi la 42. Taarifa kamili na ratiba zitawekwa katika tovuti ya Taasisi hivi karibuni.