Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo Ndugu Abdul Omar Nondoametekwa asubuhi hii na watu wasiojulikana akitokea mkoani Kigoma alikokuwa sehemu ya viongozi wa kitaifa walioongoza kampeni kwenye mikoa ya magharibi mwa Tanzania. Nondo aliwasili stendi ya Magufuli iliyopo eneo la Mbezi kwa usafiri wa basi la Saratoga lenye namba za usajili T 221 DKB
Mashuhuda wa tukio wanasema kuwa kulikuwa na purukushani katika utekaji wa Nondo iliyosababisha begi lake dogo la nguo na pingu iliyobebwa na mmoja wa watekaji kudondoka.
Pia soma: Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli
Katibu Mwenezi Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Monalisa Ndala na Afisa wa Harakati na Matukio Taifa Ndugu Wiston Mogha waliofika mapema kituoni hapo walitambua haraka kuwa aliyetekwa ni Abdul Nondo kwa sababu walizitambua nguo zake kwenye begi lililodondoka na notebook yake.
Chama kinaendelea kufuatilia taarifa zaidi kuhusu tukio hili na kitatoa taarifa zaidi kwa umma.
Katika hatua ya sasa tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Cammillus Wambura kufuatilia haraka tukio hili na kuhakikisha Ndugu Abdul Nondo anaachiwa huru mara moja.
Imetolewa na:
Mbarala Maharagande,
Naibu Katibu wa Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi,
ACT Wazalendo.
01 Desemba, 2024.
KUTEKWA KWA MWENYEKITI WA NGOME YA VIJANA NDUGU ADBUL NONDO