DOKEZO Taarifa ya madai ya udanganyifu wa mitihani na tuhuma za rushwa katika Murgwanza Institute

DOKEZO Taarifa ya madai ya udanganyifu wa mitihani na tuhuma za rushwa katika Murgwanza Institute

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mdau, kuna madai mazito yanayohusu Murgwanza Institute, chuo cha elimu ya kati kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Kagera, kilichopo Wilaya ya Ngara.

Inadaiwa kuwa wakati wa mitihani ya Supplementary End Semester II ya mwezi Desemba 2025, iliyofanyika katika Taasisi ya Rubya kama kituo cha mtihani, Mkuu wa Chuo, Anna Jackson, alitoa rushwa ya shilingi 700,000 kwa msimamizi wa mtihani kutoka wizara, Dr. Adinan Chimoto, ili wanafunzi wanne waliokuwa wamefeli somo la Pathology Level 4 (CMT) wapatiwe matokeo ya ufaulu.

Kwa mujibu wa madai hayo, taarifa zilifikishwa kwa vyombo mbalimbali, ikiwemo Usalama wa Taifa, PCCB, Wizara ya Afya (MOH) na NACTVET. Inadaiwa kuwa uchunguzi ulifanyika na kubaini tofauti kati ya alama zilizokuwa kwenye nyaraka za awali za mitihani na matokeo yaliyokuwa kwenye mfumo wa NACTVET.

Hata hivyo, kinacholalamikiwa ni kwamba hatua zilizochukuliwa ziliishia kufuta matokeo ya wanafunzi hao wanne pekee, huku taasisi, viongozi wake na wahusika wanaodaiwa kuhusika na vitendo hivyo wakiachiwa bila kuchukuliwa hatua za kisheria au kinidhamu. Aidha, kuna madai kuwa matukio mengine ya udanganyifu yameendelea kuripotiwa chuoni hapo bila hatua stahiki kuchukuliwa.

Tunatoa wito kwa NACTVET, PCCB na Wizara ya Afya kutoa ufafanuzi kuhusu madai haya na hatua zilizochukuliwa. Endapo madai haya ni ya kweli, ni muhimu uwajibikaji ufanyike kwa wote wanaohusika ili kulinda uadilifu wa mfumo wa elimu ya afya na kuhakikisha wataalamu wanaohitimu wanakidhi viwango vinavyohitajika kwa usalama wa afya za wananchi.
 
Duh halafu Afya haitakiwi haya mambo,ndo maana now kuna watumishi wengi hakuna kitu.
 
Back
Top Bottom