Taarifa ya polisi mlipuko Arusha; Victor Ambros kufikishwa mahakamani

afsa

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
1,986
Reaction score
1,585
MAJINA YA WATUHUMIWA WALIOACHIWA HURU PAMOJA NA RIPOTI YA POLISI KUHUSU BOMU LA ARUSHA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MAENDELEO YA UPELELEZI WA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI JIJINI ARUSHA LILILOTOKEA TAREHE 05/05/2013


Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba mara ya mwisho nilipokutana nanyi niliwaahidi kwamba nitaendelea kuwapa mara kwa mara taarifa juu ta maendeleo ya upelelezi wa tukio la mlipuko wa bomu lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine kudhaa kujeruhiwa.

Kama nilivyowaeleza hapo awali, baada ya tukio hilo jumla ya watuhumiwa tisa(9) walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani. Watuhumiwa haoa ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)

Raia hao wa kigeni walikamatwa pamoja na wenyeji wao wawili ambao ni raia wa Tanzania wenye asili ya Yemen. Majina ya watanzania hao ni Mohamed Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak (29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni jijini Arusha.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya upelelezi ukihusisha taaasis nyingine za upelelezi FBI pamoja na INTERPOL kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani umebaini kuwa raia hao wanne wa kigeni hawakuhusika katika shambulio hilo.

Baada ya jalada la tukio hilo kufikishwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Arusha – divisheni ya mashtaka imeelekeza kuwa watuhumiwa hao wakabidhiwe ofisi za idara ya uhamiaji mkoa wa arusha ili kuona kama kuna taratibu zozote za kiuhamiaji ziikiukwa na wageni hao wakati walipoingia nchini ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Pia ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imeandaa mashitaka dhidi ya victor S/O Ambros kalisti na amefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za mauaji na kujaribu kuua. Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa waliosalia unaendelea kwa sasa tunao wataalamu kutoka kenya na Uganda ambao tunashirikiana nao katika upelelezi wa shauri hilo.

Aidha, hadi sasa idadi ya majeruhi wa tukio hilo la mlipuko wa bomu wanaoendelea kupata matatibabu katika hospitali mbalimbali ni 31 ambao kati yao 19 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa mount Meru arusha, 4 katika hospitali ya St. Elizabeth arusha na wengine 8 katika hospitali ya taifa muhimbili jijini dar es salaam na taarifa zinaonyesha hali zao zinaendelea kuimarika.

Hata hivyo jeshi la polisi linaendelea kufuatilia taarifa za watuhumiwa wengine wanaohusishwa na tukio hilo ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani pia jeshi la polisi linaendelea kuwaomba wananchi au raiayeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kubaini mtandao wa kigaidi nawatuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo wajitokeze na kuwasilisha taarifa hizo; tayari mkuu wa jeshi la polisi (IGP) amekwishaahidi zawadi nono ya Tshs. 50,000,000/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa hizo za siri kwa kukamatwa kwa watu hao.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
LIBERATUSI SABAS – ACP
TAREHE 13/05/2013.
 
Mimi ata sielewi wanmanisha FBI wameshindwa sasa wanaona watumie wakenya na waganda ambao kenya kila mwezi lzaima kuna mlipuko ,,,,,! polisi tz so wess! stupid intelenjinsia
Kazi imeanza
 
Hehehee haya twendeni,

Mpaka ccm itoke madarakani tutaona mengi ya ajabu!
 
Kwa nini wageni hao walikamatwa na kuhusishwa na kadhia hiyo? Serikali iko tayari kuwalipa fidia kwa kuwachafua kwa tuhuma zisizowahusu? Kwa nini walikamatwa wao badala ya wengine waliokuwa eneo la tukio? Watz tuna maswali mengi juu ya jambo hili na tunaelekea kuamini maneno ya Card Pengo
 
Wale wageni wa Saudia leo si wameachiwa huru jamani?

Yericko Nyerere kama ulivyokwisha kusema kweli ya kwamba mpaka hawa mafisadi wang'oke madarakani hakika tutaona na kusikia mengi!

Mmmmmh!
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini wageni hao walikamatwa na kuhusishwa na kadhia hiyo? Serikali iko tayari kuwalipa fidia kwa kuwachafua kwa tuhuma zisizowahusu? Kwa nini walikamatwa wao badala ya wengine waliokuwa eneo la tukio? Watz tuna maswali mengi juu ya jambo hili na tunaelekea kuamini maneno ya Card Pengo
 
kuna kila dalili yule mropokaji wa arusha akakamatwa . ngoja F.B.I wamalize kazi ndio ukweli utawekwa wazi.
Pale FBI watakapotoa mchoro unaofanana na yeye, ndiyo sinema nyingine itakapoanza.
 
hili ni changa la macho,hiyo zawadi nono ya mwema pelekeni mkawatengenezee madawati watoto wetu wanaokaa chini huko mashuleni.

Haa haa haa, unajua hawa jamaa akili zao ni ndogo sana! Wanasema watatoa zawadi kwa taarifa ya wahusika wengine wakati ''mhusika'' watampeleka mahakamani. Kwanini yeye asiwatajie ni nani alioshirikiana nao? Huyu Victor hahusiki na hawa vilaza wanacheza usanii tu.
 
Huyo Victor wamemuonea tu!kama wamekosa watu wa kuwashika,wangesema upepelezi unaendelea,huyo Ambrose hana kosa!kumpa kesi mauaji ni kumuonea!
 
Hebu polisi kuweni serious kidogo, mmemshitaki Victor Ambros kwa mauaji at the same time mnasema wananchi tuwasaidie kumpata muuaji. Hapo sasa mnataka tuwaeleweje? sijui kama mnajua kuwa mna-implicate kwamba victor hajahusika?
 
Huyo Victor wamemuonea tu!kama wamekosa watu wa kuwashika,wangesema upepelezi unaendelea,huyo Ambrose hana kosa!kumpa kesi mauaji ni kumuonea!

nafasi ni yako sasa kumtaja mtuhumiwa kuna mil 50 zinakungoja mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…