Hata uamuzi wa Kamati una mapungufu makubwa sana;
1. Badala ya ku-establish facts, jamaa ana kadi au hana, wao wanatuletea habari ya matokeo!
Nani aliulizia issue ya matokeo.
2. Badala ya kutueleza kama uchunguzi uanonesha Fakhi alikuwa na kadi 2 au 3 (idadi) wao wametuletea sababu iliyosababisha akapata. Eti wanasema ripoti moja inasema alipewa kadi kwa kosa la kumvuta mchezaji mwenzake, mwingine akasema ni kwa kumrukia mwenzie. Sasa utata hapo ni sababu ya kadi au uwepo wa kadi?
3. Badala ya kuchunguza na kuestablish facts, wao wanatoa uamuzi kwa kuangalia benefit of doubt!
4. Badala ya kutueleza usahihi wa taarifa na takwimu za maafisa waliosimamia mchezo, wao wametueleza taarifa zilitumwa kwa email, mara binafsi, mara simu ilipotea, so what?
Ndio maana tunasema Malinzi, na TFF yake pamoja na kamati wamepoteza kabisa legitimacy ya usimamizi wa mpira. Waamuzi na Kamisaa hawaelewani, Kamati kwa kamati zinakuja na uamuzi tofauti kwenye jambo moja, and so forth.