Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Ndugu, Waandishi wa Habari
Mtakumbuka kuwa katika Mwaka wa Fedha 2022/23, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani alitoa msamaha wa riba ya malimbikizo ya pango la ardhi ambapo wananchi walio na malimbikizo walipewa nafuu ya kulipa deni la msingi ili wasamehewe riba ya malimbikizo kuanzia Julai hadi Disemba, 2022.
Ndugu, Waandishi wa Habari
Katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Disemba 2022, Wizara imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 90.9 sawa na asilimia 75 ya lengo la makusanyo ya Shilingi Bilioni 121. Makusanyo kwa mwaka wa fedha 2022/23 yameongezeka kwa Shilingi bilioni 33.9 ikilinganishwa na kipindi kama hiki kwa mwaka wa Fedha 2021/22.
Aidha, Wananchi 6,211 wamenufaika na msamaha wa riba ya malimbikizo sawa na shilingi 11,931,537,409.80. Serikali inaamini kuwa fedha hizo zilizosamehewa zimeenda kuleta nafuu kwa wahusika na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii nchini. Niuchukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt Samia Suluhu Hassani kwa uamuzi wake wa kusamehe kiasi kikubwa hicho kwa lengo la kuwaondolea mzigo wa madeni wananchi na taasisi mbalimbali.
Natumia fursa hii kuyapogeza mashirika ya TANESCO, CHUO CHA USHIRIKA MOSHI, MBEYA CEMENT TPDC, Hifadhi ya taifa ya chakula, kwa kuitikia kikamilifu wito wa Mhe. Rais.
Ndugu, Waandishi wa Habari
Pamoja na mafaniko yaliyopatikana katika utekelezaji wa mkakati huu, zipo changamoto mbalimbali zilijitokeza zikiwemo:-
Kushindwa kukamilika kwa baadhi ya miamala ya wananchi waliokuwa tayari kulipa deni la msingi ili wanufaike na msamaha wa riba uliotolewa na Serikali;
Changamoto ya mtandao iliyosababishwa na wamiliki wengi waliokuwa wakitumia njia za ki-eletroniki kulipa kodi kwa wakati mmoja; na Kuchelewa kwa utekelezaji wa msamaha kutokana na mchakato wa utengenezaji wa Kanuni(Tangazo la Serikali Na. 537B la tarehe 31 Agosti,2022).
Kufuatia hali hiyo, baadhi ya Taasisi za Serikali/ Mashirika ya Umma na wananchi wengi wameendelea kuwasilisha maombi ya kuongezewa muda ili kunufaika na msamaha wa riba uliotolewa na Mhe Rais.
Ndugu, Waandishi wa Habari
Naomba nichukue fursa hii kuwajurisha kuwa Mheshimiwa Rais ameridhia kuongeza kipindi cha msamaha hadi April, 2023. uamuzi huo umefikiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo maombi mengi ya wananchi na taasisi yaliyoifikia Serikali.
Hivyo, Natoa rai kwa taasisi na mashirika ya umma na wananchi wote kutumia muda uliotolewa hadi April 30 na Mhe. Rais kunufaika na msamaha wa riba uliotolewa na Serikali kulipa deni la msingi (principal amount) ili wasamehewe riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi.
Ndugu, Waandishi wa Habari
Pia, naelekeza “Ofisi zote za ardhi nchini kutoa huduma siku zote hadi mwisho wa mwezi aprilkila ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za ukadiriaji kodi kwa wakati. Aidha, nawasihi wananchi kuendelea kutumia njia za ki-elekroniki ambazo pia zimeanza kutolewa na Benki washirika za CRDB na NMB katika kukadiria na kulipa kodi ”.
Ndugu, Waandishi wa Habari
Wajulisheni wananchi kuwa Mhe. Rais ameongeza muda wa msamaha wa riba ya malimbikizo. Aidha, Wizara imejipanga kuwahudumia kikamirifu ili kuwawezesha wananchi kupata nafuu ya msamaha wa riba ya kodi ya pago la ardhi iliyotolewa na Mhe. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani.
Pia napenda kusisitiza kwa wananchi, mashirika na kampuni ambazo hazita tumia fursa hiyo Wizara imejipanga kuchukuwa hatua za kisheria kukusanya kodi pamoja na malimbikizo. hatua hizo ni pamoja na ubatilisho wa milki, kuwafikisha mahakamani kukamata mali na kunadi ili kufidia kodi husika.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.