mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,778
- 7,145
Wana JF
Nimekusanya taarifa za kiuchunguzi katika mikoa mbali mbali hasa inayolima ndizi.
Baada ya ujio wa upandaji miti ya mbao aina ya patula pine (pinus patula) nimegundua vitu vingi vimeanza kupotea kutokana na watu wakidhani wameyakabili maisha kwa kupanda miti hii baadae wauze mbao wapate fedha zilizoshikana wafanye mambo mengine, kumbe wameingia mkenge kwa kuharibu ardhi yenye rutuba na kupoteza uoto wa asili.
Miti hii hupandwa mwezi wa tisa ili Ije ikutane na mvua ya mwezi wa nne. Wanafanya hivyo kuepuka miti kupinda au kudumaa. Miti hii hupandwa kavu kavu baadae hulishwa mbolea ya chumvi chumvi iamke kwa haraka.
Sababu ya kwanini nasema uharibifu wa uoto wa asili na ukaribishaji wa jangwa ni hivi:
Tamaduni za asili ya watu wanaolima ndizi na kahawa hutegemea vitu vifuatavyo, nyasi kwa ajili ya matandaza, mifugo kwa ajili ya mbolea ya mboji au mbolea asilia. Kwa sasa vitu hivi vimekuwa adimu baada ya ujio wa miti aina ya pine
Madhara yatokanayo na pine
Pine ni mmea ambao hutoa mbao nyepesi. Majani yake huchukua takribani ya miaka mitatu kuoza. Majani haya hayana utamaduni wa kuwa rafiki wa wadudu wanaoozesha majani kwa ajili ya kurutubisha ardhi. Wadudu wanaotengeneza afya ya udongo kama minyoo asili, sisimizi na vipepeo wanaodhalisha viwavi wote wamepotea hivyo ardhi husika kukuta imaharibika.
Uchunguzi wa awali unaonyesha sehemu waliokaribisha miti hii kwa wingi wamepoteza mifugo mingi ambayo ilihusika kutengeneza afya ya udongo. Ng'ombe /mbuzi /kondoo ni wanyama wenye faida wanapokuwa malishoni. Kinyeshi Chao hutumika kama mbolea inayotegemewa na majani na mimea mingine midogo midogo lakini pia wadusus wanaopaa wanaozungusha kichezi wameisha. Wadudu hawa ni maalum kwa kusambaza mbolea wanapokuwa kwenye harakati ya kwenda kuhifadhi chakula ardhini. Sehemu ambayo mkulima huvuna mbao kwenye miti hii hukuchukua miaka mitano ukiweka mbolea ya asili kurutubisha ardhi uweze kulima kitu kingine.
Madhara yatokanayo na kilimo hiki
Sehemu ambayo wamebaki na ardhi ndogo kama Kagera na kilimanjaro wamepata hasara kubwa kwa kilimo mbadala kama mahindi, njugu mawe, viazi vitamu, magimbi, njugu mawe, karanga na alizeti. Ukosefu wa malisho kwa wanyama asili. Hivyo ongezeko la lishe duni linalotokana na ukosefu wa maziwa , nyama na mafuta ya wanyama na mimea kama alizeti mihogo na karanga.
Kagera ni mwathirika namba 1 kwa kuwa ardhi iliyokuwa inatumiwa na watu maskini kwa ajili ya kulima mazao mbadala kujikimu na maisha ardhi yote imatwaliwa. Ardhi hii iliachwa na mababu kwa ajiri ya malisho na watu kulima mazao ya muda mfupi. Kwa sasa hivi kagera kuna marumbano ambayo yanaweza kuleta mapigano kati ya wafugaji na wakulima.
Niwaombe wizara ya kilimo wakutane na wizara ya mifugo wafanye kampeni ya kupunguza miti hii lakini pia ardhi ya vijiji na shule ambayo imelimwa miti hii iondolewe watu wapate malisho na mazao mbadala