Taarifa za mikopo midogo midogo ya kibiashara!


mkuu huna mtaji unataka ukopeshwe?
unafanya hatari na utafilisika miezi michache tu.
inatakiwa uwe na zako ndio uongezee na za bank na uwe na uzoefu na biashara yako.
ukiwa na mtaji wa m10 unaweza kukopa m3 na ukarejesha bila tatizo!
 

dhamana inakuwa je hapa?
 
watu wengi wanalalamika riba kubwa,lakini imekuwa kama sheria ya uchumi kuwa interest>inflation, kushusha interest,gvt lazima inflation kwanza
 
Taarifa nyingine ni kwamba TIB wanatoa mikopo mikubwa ya uwekezaji kuanzia USD 150,000. Nitafuatilia kujua masharti yao!
Asante kwa taarifa mkuu, mimi nina biashara yangu ndogo inaendelea ninahitaji mkopo ili kuikuza lakini nina shamba tu halina hati lakin ninaweza kupata mkopo kwa dhamana hii? kama ninaweza ni bank gan watakao weza kunisaidia? Naombeni msaada wenu juu ya hili.
 


Sina hakika kama shamba ambalo halijapimwa na kwa hiyo halina hati linaweza kutumiwa kupata mkopo kutoka benki. Hebu jaribu kutembelea benki yoyote uwaeleze. Naamini watakupa ushauri na kukuelekeza cha kufanya!
 
Mimi nimezunguuka kama benk nne ila kutokana na muundo wa biashara yangu benk zote nimeka mkopo sijaelewa kwa nini awajaweka mikopo ya aina hii.hata kama una unadhamini wauwakika(NYUMBA) labda bwana MZUZU utujuze kwa TIB. Ninaotoa bidhaa na kushusha kwenye godauni au kufikisha kwa madalali.
 
Benaire kuwa mkweli, interest za access Bank, minimum ni 3.75% per month sasa unaposema 21% per annual unadanganya.
 
 
 
 
 
Usijaribu kukopa huko labda uwe na tatizo kubwa na bank uwe haukopesheki.(fanya uchunguzi wa kina kwanza kabla ya kuingia huko FINCA)

Mkuu Sanja tunashukuru sana kwa ushauri wako. Pengine kwa faida pana ya wadau jamvini, unaweza kueleza japo kifupi sababu zilizopelekea hitimisho lako? Tunatanguliza shukrani za dhati!
 
Mkuu Sanja tunashukuru sana kwa ushauri wako. Pengine kwa faida pana ya wadau jamvini, unaweza kueleza japo kifupi sababu zilizopelekea hitimisho lako? Tunatanguliza shukrani za dhati!
Kidogo ninachoweza kueleza nikuwa hiyo riba ya 5% ni kwa mwezi, sasa fikilia unachukua mkopo wa miaka mitatu (miezi36), hii inamana utatoa kiasi cha riba ya (36*5=180%) Mf umekopa 1,000,000/=, utaripa riba ya tsh50,000/= mara miezi36 jumla ya riba tu ni tsh 1800,000/= .Kama nimekosea watalam watanirekebisha. Swali linabaki nibiashara gani yenye kiasi kikubwa hivo. (Kwenye mabenk navoelewa ni riba ya muda wote wa mkopo mfano 22%)
 

Sanja umesema sana c kdg kwani umemaliza kila kitu. Catch hapa iilikuwa kwenye interest rate, jamaa aliposema 5% hakusema ni monthly rate kitu ambacho c fair. Banks zetu zinalaumiwa sana kwa riba kubwa but kwa hili la Finca then banks bado ziko better tena by far. Once again thanks Mkuu Sanja!
 

Nashukuru ndg..sasa kwa sisi tulio mbali (Mtwara mjini)tunaweza kumeet condition zako. Kama inawezekana basi ni PM tufanye kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…