Taarifa za mikopo midogo midogo ya kibiashara!

Kama kuna habari zaidi tunaomba utuwekee hapa.

Kwa mfano, wanahitaji security ya namna gani, amount wanayotoa, interest rates na kama wanakubali kutoa katika form ya overdraft.

Tutashukuru sana kwa kutuelimisha.


TIB awa hapa,kwenye mikopo ya kilimo




Na kwa ajili ya SMEs maelezo aya hapa

 

Katika hili kwa wasio na mitaji bora waungane na kuanzisha vikundi vya Hisa - ndo mkombozi wa wanyonge wanaoaminiana.
 
habari wadau? nina mradi wangu mdogo nimeshainvest fedha kazaa nimekwama 1.5 mil, ili uweze kuanza...msaada wadau wapi ntapata pesa.
biashara yangu ni mpya na dhamana nilizonazo ni vitu vya ndani.please wadau.
 
Wapi mkopo usio na riba unaweza patikana?
Nlipata kusikia ktk redio flani ila ckuipata vizuri...kama kuna mdau ana taarfa yoyote atujuze hapa.
 
Wapi mkopo usio na riba unaweza patikana?
Nlipata kusikia ktk redio flani ila ckuipata vizuri...kama kuna mdau ana taarfa yoyote atujuze hapa.


Sijawahi kusikia lolote kuhusu mkopo ambao hauna riba...

Kama kuna mtu anajua basi itakuwa vizuri tukafahamishwa. Ila nitakuwa na wasi wasi sana mkopo wa namna hiyo kwani siamini kama kuna mtu anaweza kukupa pesa yake utumie tu bila yeye kupata kitu kutoka kwako!
 
dah! Wenzetu wameendelea, kibongo bongo wanaona kumlipa mtu hadi afe itachukua muda na watapata hasara. Kuna strategies nzuri za mafanikio tunaishindwa hata kuiga!

Ukweli hilo linawezekana sababu malimbikizo ya pesa za kustaafu huwa hazifukiwi shimoni, zipo kwenye mzunguko kibiashara na sasa hivi majengo makubwa yanayoibuka kama uyoga jijini Dar ni kutokana na pesa hizo. Investiment hiyo faida yake ya miaka nenda rudi na ndizo pesa za kuwalipa kwa maisha hadi wanapokufa. Ingawa hazifikii kama dau la mshahara, hata hivyo kiwango cha chini kingekuwa walao kupata laki moja na nusu kwa mwezi kwa maisha yote mpaka kifo nadhani ingeondoa ukakasi unaowapata wengi kuishia maisha ya dhiki kama hawakufanya kazi wakati walichangia mifuko yao.
 
Just curious, ni benki gani hiyo ya Marekani iliyokuambia secured money wanatoa free under one year period?

Bank nyingi ikiwemo Bank of America, Green Bank, Wachovia, nk.

Secured money loan inamaanisha kama unakusudia kuanza mradi wa Milioni 10 na unazo hizo cash mfukoni, badala ya kutumia pesa yako hiyo unaiweka bank kama dhamana na ukawa unachukua pesa bank kwa dhamana ya pesa uliyoweka bank na hutatozwa cho chote kwa mwaka mmoja. Baada ya mwaka mmoja riba itaanza kupanda kidogo lakini si sina ni shauri ya gharama za bank zaidi. Kinachotakiwa chukua pesa hizo bank tumia na kisha rudisha, thats all.

Hili ni jambo zuri, badala ya kuchukua pesa yako na kuitumia moja kwa moja, unaweza kuiweka bank kama dhamana na ukawa unachota pesa bank kuendeshea biashara yako. Wenye nafasi nzuri kipesa hufanya hivyo.
 
Ahsante sana,

Nitawafuatilia ili taarifa zao niziweke hapa pia...Ila niliwahi kuongea nao na walionekana kana kwamba wanatoa mikopo ya chini ya 10m...Kwa mkopo ambao ni zaidi ya hapo, walionekana kupwaya!!

Napingana na wewe kuhusu Accessbank.
1; Kwa mteja mpya anaqualify kupata mkopo wa 100k-25Mil...and maximum maturity is 12months.

2;Kwa mteja anayerudia (repeat client)....upande wa micro loans bado anaqualify up to 25Mil....ila maturity ni up to 24months.

3;Pale kariakoo branch...wanakitengo cha SME...hawa wanatoa mikopo from 30Mil and above!

4;Interest ya Accessbank ni 21%,Loan processing duration ni 3days.

NB; Wako active sana kwa mtu asielipa kwa wakati otherwise masharti yao ni nafuu sana.
 

Hata hapa Tanzania kuna bank ambazo zinaruhusu mteja kufungua Fixed deposit account.....then ndio inakuwa dhamana ya mkopo wake!
The same thing!
 


Ahsante sana Mkuu,

Hata hivyo, hiyo interest rate ni kubwa sana kulinganisha na mabenki mengine!
 
Mie nimeshajenga frames huku bara, hapa nimekwama pesa ya kianzio tu yaani 2m ambayo nitaitumia kwa aina ya biashara. Ninazo dhamana zisizohamishika japo HATI ndio bado sijaipata, sijaanza biashara ila ndio natarajia kuanza.

Wapi nitapata mkopo? Maana nimewaona Access Bank wao wanasema wanatoa mikopo kwa walio na biashara tayari, nimeshindwa nifanyeje nipate kujikwamua kiuchumi.
 
access bank nilikopa 5m narejsha 565,000 mwezi wa tisa huu nikimaliza watapata 1,780,000 ni %hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…