Amini usiamini, hii ya kupewa kwa mkupuo kwa wengi ni mbaya sana, kwani unavyoona we unaweza kurudufu pesa yako hadi utakapokufa si wote wenye uwezo na upeo huo. Hata kama watapewa mafunzo ni sawa na shule wanaokuja kufauulu ni mmoja au kushindwa wote. Mataifa yaliyoendelea yanatoa mafao hayo kwa utaratibu wa kupewa kila mwezi na hii hadi kifo kitakapomchukua, hii inamhakikishia kupata kila mwezi au kila baada ya miezi miwili.
Pato lake hilo ni msaada pia kupata mkopo kama anataka kuanzisha biashara kwa kuwa ni income ya uhakika ambayo itampa dhamana bank kupata mkopo wenye riba nafuu. Kumbuka mataifa makubwa wamefanya utafiti wa miaka mingi na wameishia kuwalipa kwa mzwei badala ya kwa mkupuo ktuokana na wengi kuishia kuwa homeless.