JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Taarifa za kudukuliwa na kuuzwa kwa data ilichapishwa mara ya kwanza na tovuti ya utafiti ya Cybernews ya usalama wa kitandao tarehe 7 Aprili, 2021 ikisema kuwa, taarifa zilizodukuliwa ikiwa ni pamoja na jina la utambulisho, barua pepe, namba za simu, jinsia, vyeo vya kitaalamu, na kiambatanisho cha mitandao ya kijamii mingine zimeuzwa katika jukwaa hilo.
Kwa mujibu wa LinkedIn wameeleza kuwa hifadhidata kwa ajili ya mauzo ni mkusanyiko wa data kutoka kwa idadi ya tovuti na kampuni. Data kutoka kwa watumiaji wa LinkedIn inahusisha taarifa pekee ambazo watu wameziweka wazi katika akaunti zao, tovuti za kitaalamu za mitandao ya kijamii zinazomilikiwa na Microsoft.
Upvote
1