Hazard CFC
JF-Expert Member
- Apr 7, 2015
- 16,627
- 38,689
TAARUKI MSIMBAZI, WAANZA KUTOFAUTIANA NA MWEKEZAJI
Na SaleheJembe
Hali ya sitofahamu imeanza kutokea huko MSIMBAZI baada ya MWEKEZAJI wao kuanza kutofautiana na Viongozi wa Club
Kiongozi mkubwa wa wanamsimbazi ameongea na Salehe Jembe leo(Jana) akitoa malalamiko juu ya MWEKEZAJI kutaka kumiliki Mali zote za Club zitakazoanzishwa chini ya ufadhili wake Kwa 70% ,umiliki huo utadumu ndani ya miaka 35 hata kama club itakuwa chini ya MWEKEZAJI mwingine Kwa sababu anaamini ataweza rudisha gharama zote anazotumia kuendeshea club AMBAYO inafanya vizuri hasa Kwa Mechi ZA kimataifa.
Kulingana na kauli ya MWEKEZAJI tayari baadhi ya viongozi wa Simba wameanza kukaa vikao vya Siri pamoja na wanasheria watakaotumika kumng'oa MWEKEZAJI kisheria mapema kabla madhara hayajatokea maana hii ni timu ya Wananchi na kila mwanasimba ana haki ya kuwekeza ili aweze kunufaika na si kumpa MTU mmoja amiliki kwa asilimia nyingi bila sababu zozote.
Kwa habari za chinichini inasemekana kuwa wazee wa Simba walifanya KIKAO na MWEKEZAJI NYUMBANI kwake wakimuomba asifanye hivyo maana club inamtegemea Kwa sasa na wapenzi wanampenda kutokana na mafanikio waliyoyapata Kwa muda mfupi.
Baada ya KIKAO na wazee wa Simba inasemekana MWEKEZAJI hajakubaliana nao maana yeye yupo kimaslai zaidi maana PESA zinazotumika kuendeshea club zinatoka kwenye vyanzo vingine ndani ya Kampuni zake.
Kwa sasa viongozi wa Msimbazi wapo kwenye mchakato wa kumtafuta MWEKEZAJI mwingine mapema iwezekanavyo ili kuepusha club kuingia kwenye ukata mkubwa kama ilivyotokea Kwa watani wao Yanga ambao wanaishi Kwa kutegemea michango ya wanachama maana MWEKEZAJI ametishia kuvunja MKATABA iwapo kama watashindwa kuafikiana.
Anaripoti SaleheJembe.
Sent using Jamii Forums mobile app