Uchaguzi 2020 Taasisi iliyokusanya maoni ya mgombea wa CCM kushinda uchaguzi mkuu kwa asilimia 85, inachekesha na kusikitisha

Course Coordinator

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2019
Posts
1,742
Reaction score
3,224
MAANA YA UTAFITI
Utafiti ni njia ya kupata utatuzi wa suala fulani katika jamii na mazingira ya binadamu kwa njia ya uchunguzi unaotumia nadharia za kitaaluma na kisayansi.

Aidha utafiti ni njia maalum inayofuatwa ili kufikia ujuzi au taarifa muhimu inayokusudia kuchangia katika usomi wa kina na uchunguzi wenye mweleko wa kimaantiki. Utafiti wowote ule hauwezi kufanyika wala haukamiliki pasi kuongozwa na nadharia kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Kuna utafiti wa taasisi ya SSRC imekuja na utafiti wa kura za maoni kuwa mgombea wap wa Uraisi atashinda kwa 85% maoni hayo ni kama yaliishaminishwa huko nyuma na Katibu Mkuu wa CCM kuwa mgombea wao ataweka historia ya kushinda kwa 84% hivyo utaona hiyo taasisi haijaenda kufanya utafiti kwa kukusanya maoni kwa wapiga kura isipokuwa imechukua maoni ya katibu mkuu ya kutaka kulazimisha ushindi huo wa kushindo bila kuzingatia matakwa ya wapiga kura.

Nini dhana ya utafiti, Utafiti umeelezwa kwa njia mbalimbali.

Ufafanuzi mpana wa utafiti unatolewa na Godwin Colibao "Katika maana pana zaidi ya neno, ufafanuzi wa utafiti unahusisha kukusanya mambo yoyote ya data, habari na ukweli kwa ajili ya kuendeleza ujuzi.

Ufafanuzi mwingine wa utafiti unatolewa na John W. Creshwell ambaye anasema "ni mchakato wa hatua za kukusanya na kuchambua habari ili kuongeza uelewa wetu wa mada au suala". Inajumuisha hatua tatu ili kuuliza swali, kukusanya data ili kujibu swali, na kutoa jibu la swali.

Uongo wa Utafiti wa CCM
haulezwi umechukuliwa sehemu gani mkoa gani? Haulezwi ni idadi gani ya watu wangapi na makundi gani, umri na elimu zao, jinsi zao?

Haulezi ni vigezo wametumia kufanya utafiti aina ya maswali kama ni ya wazi au lah (wasije wakawa wanauliza unaonaje MAGUFULI atashinda Urais) halafu wanauliza makada wa CCM.

Ukweli ni kuwa kabla ya utafiti kulikuwa na ramli chonganishi huo unaoitwa utafiti wa Polepole ni ramli chonganishi.

Kwa vyovyote vile uwanja ukiwa huru hakuna mgombea atakayevuka 57% ya ushindi. Ushindani wa mwaka huu ni mkubwa.

Moja Rais aliyeko madarakani huwa anachokwa hivyo lazima asilimia zishuke tena kwa Meko zitashuka sana tu. Kinachomtofautisha Meko na maraisi wengine wastaafu ni ukatili wake wa kufingia vyombo vya habari, kutoguswa na majanga makubwa ya kitaifa kama vile tetemeko la Bukoba, Watoto 32 waliofariki pale Arusha, Polisi wetu 10 waliofariki pale Kibiti, watu kupotea, kutekwa na kuteswa na upendeleo wa waziwazi kwa CHAMA chake, kabila lake na rafiki/jamaa zake wa karibu nina imani CHADEMA wangetoa tafiti NBS leo wangekifungia hicho chombo kilichofanya utafiti.

Week end njema kwa Wote.
Jumamosi njema kwa wote.
 
Mwaka huu CCM inashinda kwa asilimia 95
Hata wakipiga wa kijiji chake cha Chato hafikishi 70 asimilia .
Kwenye Uchaguzi 2010 alishindwa kupata hiyo 95 akaambulia 61 pale chato na mwka huu shangaz Husna anapiga nondo kwelikweli
 
Yaani mtu aliyeshinda kwa zengwe mwaka 2015 kwa 58%, miaka mitano baadae akiwa ameuvuruga uchumi, demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari vilivyo, eti ashinde kirahisi tu kwa 85%!!!

Huu ni utani wa karne.
 
Wakuu mi nataka nibet, anayeamin Lissu atashinda aweke Laki tano mi niweke million , akishinda anachukua Million akishindwa mi nachukua laki tano yake, chap washabiki wa Chadema mje ..hatutak maneno tunataka vitendo
.
 
Yaleyale ya Belarus.Rais anatangazwa mshindi kwa 80%, then vichwa vinajaa na kufunga barabara. Then unajiuliza hao waliompigia kura 80% ni wepi?! Mbona wote wamejaa barabarani?!!
Ndio hapo tunahoji utafiti na ramli chonganishi. Toka mwanzo Bashiru anasema Magufuli anashinda kwa 84% unajiuliza hata wagombea hawajateuliwa kuingia kwenye mchakato anashindaje?

Kizazi cha mwaka 1992 hadi 2002 asilimia 80 wanahitaji CCM ibadilishwe itoke madarakani sio kwamba hawaipendi ila hawajawahi kuishi nayo sio rafiki kwao.
Sisi wa 1970-1990 ni 50/50 saa unajiuliza ashinde vipi
 
Wakuu mi nataka nibet, anayeamin Lissu atashinda aweke Laki tano mi niweke million , akishinda anachukua Million akishindwa mi nachukua laki tano yake, chap washabiki wa Chadema mje ..hatutak maneno tunataka vitendo
.
Mkuu hakuna aliyesema kuhusu ushindi tumesema kuhusu utafiti wengine ni dini zetu kubeti ni machukizo.
Tunachoongoa ni ramli chonganishi za pole pole.
 
Mwaka huu CCM inashinda kwa asilimia 95
Nimeamini jina linabeba hatma ya mwenye jina, ndio maana imeandikwa mpe mwanao jina jema. Hivi ukimuita mwanao jalala unategemea asinuke kweli? Ukijiita jingalao unategemea uwe janjalao? Na mti hujulikana kwa matunda yakw
 
Wewe endelea kuelewa hivyo ila UKWELI mchungu ni huo huo CCMinakwenda kushinda kwa zaidi ya 87% OCTOBER28.

Endelea kujipa moyo ukikariri wazungu.
 
Wakuu mi nataka nibet, anayeamin Lissu atashinda aweke Laki tano mi niweke million , akishinda anachukua Million akishindwa mi nachukua laki tano yake, chap washabiki wa Chadema mje ..hatutak maneno tunataka vitendo
.
Unajiamini kwa sababu unajua mna tume ya uchafuzi ya CCM. Unakumbuka ile kauli nikuteue mimi, nikupe gari na posho, nikupe nyumba halafu umtangaze mpinzani.
 
Hata wakipiga wa kijiji chake cha Chato hafikishi 70 asimilia .
Kwenye Uchaguzi 2010 alishindwa kupata hiyo 95 akaambulia 61 pale chato na mwka huu shangaz Husna anapiga nondo kwelikweli
2015 Team lowassa iliwabeba Chadema mwaka huu ndio mtaelewa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…