Taasisi mbalimbali kupinga kufutwa kwa matokeo kidato cha nne -2012

Taasisi mbalimbali kupinga kufutwa kwa matokeo kidato cha nne -2012

mkisyeli

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2013
Posts
260
Reaction score
76
Kwanza kabisa naipongeza tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza kuwepo kwa matokeo mabovu ya kidato cha nne mwaka 2012 je ni sahihi kwa taasisi mbalimbali zilizojitokeza hivi karibuni kama HAKIELIMU kupinga uamuzi huo na kuitaka serikali kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili sekta hiyo ya Elimu kama vile malimbikizo ya mishahara,kupewa posho,kupatiwa nyumba nzuri za kuishi pia kutumia mitaala mahususi. Katika kufundishia mashuleni
Swali,je?ni sahihi kwa Taasisi hizi za Elimu kupinga kwa kufutwa kwa matokeo haya ya kidato cha nne??
 
Ni sahihii kabisa, coz hawajachunguza kwa undani zaidi yaani itaathiri kuliko ilivyoathiri matokeo mabaya.
Hayo maamuzi ya kutumia hizo GRADE mpya yangeanza kwa watahiniwa wa mwakani,cha msingi ni kuwawajibisha waliosababisha tatizo hilo.
 
Hivi jamani hata waziri mkuu hakujua kuwa upangaji(grading) wa mwaka huu ni tofauti na miaka mingine? Kwa nini ali-linganisha(constracting) matokeo ya mwaka huu na miaka ya nyuma (2007-2012) wakati kuna utofauti katika upangaji(grading)?
Au ndio siasa jamani?
 
Ni sahihi kuyapinga marekebisho ya matokeo kwani hata kabla hayajatangazwa yaliridhiwa na wizara na yakatangazwa na waziri ambaye ni serikali, kama kuna kasoro zimeonekana inapaswa wawajibishwe waliosababisha lakini kufuta matokeo sio njia nzuri ya kuboresha taaluma bali ni kumaliza tatizo kisiasa.
 
Yaa Kitendo cha kufutwa kwa matokeo taasisi zinazopinga ni zinapinga bure tu kwa maneno kwan tayari wameshafaham sababu tatu za msingi za mwaka huu kufeli hivyo wawaache wahusika watumie busara zao kubadilisha matoko kwan tayar wmeshagundua mapunguf yao tofaut na mengine.......taasisi zinapinga bure tu zinasababu zao zingine tu wanazozijua......
 
Kufuta matokeo ci logic, la msing tuutathimin mfumo wetu wa elimu na kuweza kuunda katika viwango vinavyofaa!
 
acha tu Matokeo yafutwe kwani hata hao wanao pinga kuwa yasifutwe hawana sababu za msingi na hawaangalii athari zitakazojitokeza kwa vijana wengi kushindwa kuendelea na elimu ya Advance mwaka huu.
 
mi naona kama wata tangaza atokeo mapya zaid ya yale ya awali wata sababsha kuto aminika tena na matokeo yao. napia watoe tamko kwamba wame jipanga vp ku hakikisha suala hili hali tokei tena,? ikiwa mpaka sasa hv sabab zote zilizo changia matokeo hayo mabov zina onekana kiutendaji ktk secta zote za elim..,! pia watoe tamko kwamb wata wafarij vp wana funz wa miaka ya nyuma ambao pia wana weza kua wame feli kutokana na ucmamiz m'bov kiu saishaji? na je tuta weza vp kujitoa ktk utegemez wa ktechnolojia ambao mpaka sasa 2na tegemea stik za kuchokolea meno kutoka china iki 2na uwezo wa kufanya wenyewe na wao ndo chanzo cha kukwamisha nchi? na je mabadiliko holela ya mitaala ya kufundishia ni kweli ina zingati mabadiliko ya sayanc au ni njama za kuunda majopo mengi ambao matokeo yake ni kupoteza pesa kzembe? na kama ikionekana necta ndo wana makosa wata chukuliwa hatua gani ili iwe fidia kwa kukwami shughuli nyingine za serikali.. ikiwa matokeo ya rufaa yalionekana ni mabaya zaid wata 2mia njia gan kuya rudisha wanapotaka?..... acheni ku2danganya katka secta muhmu kimasha kama elim bhana.kama mna taka pesa chukueni 2 2me shazoea kuibiwa ila 2 acheni 2some ili 2weza ku endana na hali ngum ya maisha ina kuja...asanteni
 
ni sawa kabisa kupinga kufutwa kwa matokeo, cha msingi watibu tatizo la elimu na sio kuficha tatizo.
 
Yaa Kitendo cha kufutwa kwa matokeo taasisi zinazopinga ni zinapinga bure tu kwa maneno kwan tayari wameshafaham sababu tatu za msingi za mwaka huu kufeli hivyo wawaache wahusika watumie busara zao kubadilisha matoko kwan tayar wmeshagundua mapunguf yao tofaut na mengine.......taasisi zinapinga bure tu zinasababu zao zingine tu wanazozijua......

rabda ni kupe mfano rahc ikiwa ww ni miongoni mwa wazaz waliopoteza watoto wao wapendwa baada ya watoto wao kjinyonga kutokana na matokeo ma baya halaf matokeo ya pili yaka toka ame faulu utaendelea kuipongeza ama kchukia serikali ambayo una endelea kuitetea hapo?
 
Jamani tuache ushabiki na siasa kwenye suala la kitaaluma; kurudia matokeo hayo kunamaanisha hatuna serikali na baraza la mitihani halipo. Hii ni kwa sababu baraza lilijiridhisha na shughuli nzima ya usahihishaji na wizara husika ikakagua ikabariki matokeo yakatangazwa; JE iweje matokeo yarudiwe na hao wanafunzi watakaoendelea na alama za kubebwa watakuwa na tija yoyote kwa maendeleo ya taifa? Ukweli watoto wetu walifeli na si kutafuta sababu wakati ziko wazi. Jiulize swali dogo tu UTAWEZAJE KUSIMAMIA NA KURATIBU ELIMU BILA MTAALA? PILI UTADHUBUTUJE KUBORESHA ELIMU BILA KUBORESHA MAZINGIRA YA MWALIMU KAMA MDAU NAMBA MOJA; kwa mambo kama haya ''''''no common teaching at all''''' Na matokeo lazima uyashangae tu
 
Kwqa mtazamo wangu naona hawa jamaa si sahihi kwao kupinga kufutwa kwa haya matokeo...
Kama wanaona kuna madhaifu katika elimu wangeunga mkono kwanza kufutwa kwa matokeo halafu wangekuja na solution nyingiine ya muda mrefu katika hili....
 
Ni sahihii kabisa, coz hawajachunguza kwa undani zaidi yaani itaathiri kuliko ilivyoathiri matokeo mabaya.
Hayo maamuzi ya kutumia hizo GRADE mpya yangeanza kwa watahiniwa wa mwakani,cha msingi ni kuwawajibisha waliosababisha tatizo hilo.

Wewe ni mvivu wa kufikiri kama jamaa zako unaowaunga mkono.Kama kosa ni la wizara kutumia njia mpya ya marks grading bila kuwashirikisha wadau kwa nini uwaathiri vijana wasio na hatia.Serikali imefanya jambo la busara sana hawa haki elimu nadhani hawana nia njema na vijana waliofelishwa kimakosa wao wako kupinga tu kila kitu.
 
Nadhani tukio kama hili la kufutwa matokeo linaweza kutokea Tanzania pekeyake, na hii ni kutokana na kuwa na serikali dhaifu kupita kiasi.
 
Political wise hawako sawa maana kiukweli ni kwamba wengi wa vijana waliofeli wangeishia kuililia serikali na chama na hata vyama vinginevyo kwa kushindwa kutetea maslahi yao. Hayo ndiyo maamuzi magumu ya serikali kwa manufaaa kwa wote.

Kitaalamu wako sawa kabisa maana wanachotetea siyo matokeo ya 2012 pekee bali elimu yetu kwa ujumla. Nadhani hata NECTA wako katika wakati mgumu sana ingawa kufanya remarking ni kazi rahisi mno nayo ni kuongeza maksi 14 mfano hivyo mambo ya spread sheet ni fasta tu unafyatua lakini kwenye ubora je? Hapo ndipo taasisi za kiraia wakiongozwa na Mbatia wanapopigia kelele na si pengine.

Labda tu nijiulize NECTA wako huru kiasi gani? Kabla ya waziri kusoma matokeo hakuyaona hayo/ hakuuliza vyema? Je tume iligundua tu hilo la grading au lipi jipya walilolileta kama suluhisho la matatizo ya sekta ya elimu hapa nchini?
 
Hapa n ----- tu tunafanya,
Walifeli kiukweli na hawajaonewa, hawajui kitu kabisa hata ukiwauliza maswali, mm ninao mfano hai wa mtoto wa bro, nilijaribu kumuuliza maswali ya kawaida b4 matokeo nkamtabilia kuwa asipopata 4, basi atakuwa amependele. Matokeo yalipotoka akawa na 4 ya 33, imenibidi nimpeleke arudie fomu 2 shule moja ya seminary, alipewa mtiani wa fomu 1 na 2 afanye ili alifauli aendelee na fomu 2, chupu chupu afeli, sasa uyu akiongezewa max na akafaulu unategemea fom 5 tunapeleka nn?

Pia nimeshalipa mamilioni je matokeo yakitoka amefaulu nani atanirudishia ela yangu?

Hapa kwa jirani yangu mtoto wake alikunywa sumu baada ya matokeo, je yakitoka amefaulu serikali itamsaidiaje uyu jilani yangu?

Kwanini serikali isifanye mahamuzi magumu ya kuwarudisha darasani wafanye tena mitiani mwezi wa 11?

Au serikali imeamua kujenga taifa la mazuzu?

Prof Mkandala ukikubali tutakuwa na mashaka uprof wako

Dr Ndalichako ukikubali tutakuwa na mashaka na uDr wako.

Tuache ushabiki wa kisiasa, Taifa linakufa na hawa watoto wa siku hizi hawasomi kabisaa.
 
Mimi naona hapa kuna fikra potofu kwa baadhi ya watu, kuna watu wanafikiri matokeo yakipangwa upya kwa kufuata utaratibu wa miaka yote tuliozoea basi wanafunzi wote watafaulu. Mimi naona watainiwa wa mwaka jana hawakufanyiwa fare kupandishiwa alama bila kupata taalifa yoyote kutoka Necta kwa hiyo Necta ndio wanamatatizo na sio baadhi ya wanafunzi ambao wamefelishwa na huo uamuzi wa kupandishwa kwa alama bila kuzingatia mazingira yanayomhusu muhusika kuzipata hizo alama mpya ambazo ni batili kwa watahiniwa wa mwaka jana. Ningependa kuona mtu anakuwa mwelevu zaidi kuliko kuweka ubishi mbele kwa manufaa yake binafsi kwani matokeo ya alama yakipangwa kwa kufuata utaratibu wa kawaida ni kipi kitakacho haribika? Au mnapenda kuona watu wanapata shida ya kufelishwa kwa upuuzi walifanya wachache?
 
Back
Top Bottom