Hapa n ----- tu tunafanya,
Walifeli kiukweli na hawajaonewa, hawajui kitu kabisa hata ukiwauliza maswali, mm ninao mfano hai wa mtoto wa bro, nilijaribu kumuuliza maswali ya kawaida b4 matokeo nkamtabilia kuwa asipopata 4, basi atakuwa amependele. Matokeo yalipotoka akawa na 4 ya 33, imenibidi nimpeleke arudie fomu 2 shule moja ya seminary, alipewa mtiani wa fomu 1 na 2 afanye ili alifauli aendelee na fomu 2, chupu chupu afeli, sasa uyu akiongezewa max na akafaulu unategemea fom 5 tunapeleka nn?
Pia nimeshalipa mamilioni je matokeo yakitoka amefaulu nani atanirudishia ela yangu?
Hapa kwa jirani yangu mtoto wake alikunywa sumu baada ya matokeo, je yakitoka amefaulu serikali itamsaidiaje uyu jilani yangu?
Kwanini serikali isifanye mahamuzi magumu ya kuwarudisha darasani wafanye tena mitiani mwezi wa 11?
Au serikali imeamua kujenga taifa la mazuzu?
Prof Mkandala ukikubali tutakuwa na mashaka uprof wako
Dr Ndalichako ukikubali tutakuwa na mashaka na uDr wako.
Tuache ushabiki wa kisiasa, Taifa linakufa na hawa watoto wa siku hizi hawasomi kabisaa.