Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Awali, Mdau wa JamiiForums.com aliandika kuwa Walimu wa Halmashauri ya Arusha wanatarajiwa kupewa mafunzo kwa ajili ya mitaala mipya ya Kidato cha Kwanza kwa malipo ya Tsh. 3,000 kwa siku ikiwa ni malipo ya chai, kwa maelezo kuwa yatakuwa mafunzo ya siku mbili, hivyo kila mmoja atalipwa Tsh. 6,000/=.
Kusoma zaidi kuhusu hoja hiyo bofya hapa ~ Walimu watakiwa kuhudhuria mafunzo ya mtaala mpya kwa siku 2 kwa malipo ya Tsh. 3,000 kwa siku!
Mwanachama mwingine wa JamiiForums.com akaandika “Walimu watapewa mafunzo hayo upande wa Mwanza bila kupewa fedha za kujikimu.”
Kusoma hoja hiyo bonyeza hapa ~ Walimu Mkoani Mwanza wafanya Mafunzo ya Mtaala Mpya bila Posho
Ufafanuzi umetolewa kuhusu hoja zote hizo mbili kutoka kwenye Mamlaka husika ya Serikali.
Akizungumza na JamiiForums kuhusu hoja hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba, ambao ndio waratibu wa mafunzo hayo, amefafanua:
“Kwanza ieleweke wazi kuwa mafunzo haya yanafanyika katika ngazi ya shule. Hata hivyo, kwa ajili ya kubadilishana uzoefu baina ya Walimu, shule zaidi ya mbili zinaweza kukutana katika ngazi ya kata au tarafa.
“Walimu wanapokutana katika vituo vyao wanapata mafunzo kutoka chanzo kimoja ili kuhakikisha kuwa walimu wote wanapata mafunzo yenye ubora sawa.
“Mafunzo haya yamelengwa kuwawezesha walimu kutekeleza mtaala ulioboreshwa na yamepangwa kuwafikia walimu wote wa sekondari nchini. Utaratibu uliopo ni kuwawezesha washiriki kupata chai kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa muda uliopo unatumika vema katika kutoa mafunzo tajwa.
“Mfumo huu sio tu kwa ajili ya Arusha au Mwanza bali utaratibu nafanyika hivyo kote Nchini. Mpaka sasa serikali imeshawafikia Walimu katika mikoa 23, na inatarajiwa kuwa mafunzo yatakamilika tarehe 31.1.2025.
“Mafunzo haya ni endelevu na yataendelea kutolewa katika ngazi ya shule kupitia jumuiya za ujifunzaji kwa kutumia mfumo wa ujifunzaji wa kidijitali ujulikanao kama Learning Management System yaani LMS.”