Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) yafafanua madai ya kutoa mafunzo ya Mitaala kwa Walimu bila kuwapa posho

Tumefundishwa (sijui kama tulielewa?) na ilikuwa chai tu! Kweli mlitaka tukatae jamani?
 
Haya ni matatizo ya kukariri kupewa posho kwa kila jambo.
Ni mentality mbaya kwa taifa.
Mafunzo yanayofanyika shuleni kwa faida ya waalimu bado waalimu wanataka wapewe posho.
Wewe nae ni mpuuzi tuu. Imagine mimi nimesafiri kwenda one way ni 15000 elfu times 2 ni 30000/= one day.
Na ilikuwa two days it means nimetumia 60000/= then naenda pale napata wali maharage wa 1500/= .
Kwako unaona hiyo ni sawa?????? Kisa mafunzo napewa mimi mwalimu?
Kuwa na staha ndugu.
 
Naungana na wewe kiongozi hii haiko sawa,ivi hawa watu wanajua kutoka eneo mojahadi jingine unaweza kulipia pesa nyingi zaidi ya iyo elfu 3 kwa siku?
 
Watu wamechoma nauli zao kilomita za kutosha mnadai ni ngaz ya shule? Tuambieni ni wapi mmetoa mafunzo kwa shule moja au 2 tu. Mmewaunganisha walimu shule zaidi ya 5 karibu kila halmashauri. Mliwapa taarifa hizo wahusika kuwa yako kwa utaratibu huo?
 
Haya ni matatizo ya kukariri kupewa posho kwa kila jambo.
Ni mentality mbaya kwa taifa.
Mafunzo yanayofanyika shuleni kwa faida ya waalimu bado waalimu wanataka wapewe posho.
SHule gani imefanyiwa peke yake hayo mafunzo? Na wapi walishirikishwa kuwa ilistahili kuwa kila shule ila waungane ili ku share uzoefu? Tuache siasa kwenye mambo ya msingi msifanye watu kama ni hamnazo.
 
Hao walimu watulie kabisa. Hata kwenye uchaguzi hatutawalipa.
 
Walimu wako vizuri sana kiuchumi, walichanga pesa za kuchukua fomu na kumuunga mkono mwishimiwa. Hizo posho sio shida zao jamani. Walimu ni watu wema sana Mungu awabariki!
 
Sehemu ambavyo hatutakiwi kuleta siasa ni elimu maana hicho ni kiwanda
 
Hawajapata hela ya wafadhili kwa ajili ya mtaala mpya ili wawape posho walimu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…