jumapondamali
Member
- Nov 1, 2024
- 8
- 1
Mradi wa SEQUIP - AEP unafadhiliwa na Benki ya Dunia na unatekelezwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI. Mradi huu unalenga kuwarudisha watoto wa kike waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali kupitia elimu mbadala (Alternative Education Pathway).
Mpaka sasa umepita muda wa miezi miwili mfululizo wawezeshaji (walimu) katika mradi huu hawajalipwa stahiki zao bila taarifa yoyote. Malipo yamelipwa kwa mara ya mwisho mwezi Agosti, 2024. Malipo ya mwezi Septemba, Oktoba na Novemba hayajafanyika.
Hata hivyo, tangu kuanzishwa kwa mradi huu malipo yamekuwa yakisuasua kwa malipo ya mwezi husika (yaani malipo ya mwezi wa kwanza yamekuwa yakilpwa mwezi wa pili mwishoni au wa tatu mwanzoni) hali inayopelekea walimu kufanya kazi kwa manung'uniko.
Tunaomba mamlaka husika itoe ufafanuzi juu ya malipo kwa watumishi hao kwani mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ile.